Home » News and Events » Bodi ya STAMICO na STAMIGOLD zajadili mustakabali wa Mgodi wa dhahabu wa Biharamulo

Bodi ya STAMICO na STAMIGOLD zajadili mustakabali wa Mgodi wa dhahabu wa Biharamulo

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na ile ya Kampuni Tanzu ya STAMIGOLD, zimefanya kikao kazi jijini Dar es Salaam, kujadili mustakabali wa Mgodi wa Dhahabu wa Biharamulo katika utendaji kazi wake na uzalishaji wenye tija.

Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO (aliyekaa katikati) akihitimisha kikao kazi cha siku moja baina ya bodi hiyo na ile ya STAMIGOLD, kilichomalizika jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo wajumbe walijadili mustakabali wa Mgodi wa uzalishaji Dhahabu wa STAMIGOLD-Biharamulo uliopo mkoani Kagera; changamoto zilizopo na mwelekeo wake katika kukuza uzalishaji. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa Madini nchini, kutoka Wizara ya Nishati na Madini (MEM) Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa tatu kutoka kushoto).

Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Balozi Alexander Muganda amesema kikao kazi hicho kimejadili changamoto zilizopo katika Mgodi wa Biharamulo, mbinu za kuzitatua na mwelekeo wake katika kuongeza  mapato ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

STAMICO kupitia Kampuni yake Tanzu ya STAMIGOLD, ilianza rasmi kuendesha mgodi wa Biharamulo mwezi Februari 2014, baada ya STAMICO kukabidhiwa rasmi mgodi huo na Kampuni ya Pangea Ltd, Novemba 2013. Mkuo wa kwanza wa dhahabu ulianza kuzalishwa rasmi katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo, mwezi Julai, 2014.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni Tanzu ya STAMIGOLD Dakta Jonas Lipokola akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi kilichomalizika hivi karibuni baina ya bodi hiyo na bodi ya Shirika lake mama la STAMICO. Waliokaa kushoto kwake ni Wajumbe wa Bodi ya STAMICO wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho.

Akizungumzia changamoto za STAMIGOLD, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mpya wa STAMICO, Mhandisi John Nayopa amesema ataimarisha utekelezaji wa maamuzi ya bodi ya STAMICO na STAMIGOLD ili kutatua changamoto zilizopo kwa wakati, kabla hazijaleta madhara katika shughuli za uendeshaji na uzalishaji mgodini hapo.

Kwa mujibu wa Nayopa, baadhi ya changamoto hizo ni upatikanaji wa mtaji wa kutosha wa uendeshaji Mgodi, mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mgodi na mkakati ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

PICHA BOARD 3

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO, wakiwa katika kikao kazi cha siku moja walichokifanya kwa pamoja na Bodi ya STAMIGOLD, ili kujadili mustakabali wa Mgodi wa uzalishaji Dhahabu wa STAMIGOLD-Biharamulo uliopo mkoani Kagera; changamoto zake na mwelekeo wa mgodi huo katika kukuza uzalishaji.

==============================MWISHO=============================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela
Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
S.L.P 4958,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2150029, 
Barua Pepe: info@stamico.co.tz
Tovuti: http://www.stamico.co.tz

Copyright © 2018 State Mining Corporation. All Rights Reserved.