Home » News and Events » Bodi ya STAMICO yazidi kuboresha uongozi wa Shirika ili kuimarisha utendaji kazi

Bodi ya STAMICO yazidi kuboresha uongozi wa Shirika ili kuimarisha utendaji kazi

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) imeendelea kuboresha uongozi wa Shirika hilo kwa kumthibitisha Bw. Deusdedith Magala kuwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala na kumteua Bw. Aloyce Tesha kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji.

Uteuzi huo unaanza Julai 1 2017.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bw. Hamisi Komba (aliyesimama  kulia) akisalimiana na Wakurugenzi wa STAMICO waliothibitishwa kazini na kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Bw. Deudedith Magala (aliyesimama kushoto) amethibitishwa kuwa Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, nafasi aliyoikaiumkwa miaka mitatu. Aidha Bw. Aloyce Tesha (aliyesimama katikati) ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji na Masoko.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bw. Hamisi Komba (aliyesimama kulia) akisalimiana na Wakurugenzi wa STAMICO waliothibitishwa kazini na kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hivi karibuni. Bw. Deudedith Magala (aliyesimama kushoto) amethibitishwa kuwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala. Aidha Bw. Aloyce Tesha (aliyesimama katikati) ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji na Masoko.

Kabla ya kuthibitishwa katika nafasi hiyo, Bw. Magala, ambaye aliajiriwa STAMICO kama Meneja Utawala mwezi Aprili 2014, ameikaimu nafasi hiyo kwa miaka mitatu; ambapo Bw. Tesha yeye alikuwa Kamishna wa Madini Kanda ya Magharibi kabla ya uteuzi wake.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO Balozi Alexander Muganda amesema maamuzi ya kuthibitishwa kazini na uteuzi huo, yalifikiwa kwenye kikao cha 91 cha Bodi hiyo, kilichomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Balozi Muganda amesema Bodi imefikia maamuzi baada ya Menejimenti kuridhika na utendaji kazi, uwajibikaji uliotukuka na uzalendo wa Wakurugenzi hao, katika kutekeleza majukumu yao hapa STAMICO. Hatua hiyo itasaidia kupata uongozi wenye mamlaka kamili watakaoliwezesha Shirika kujiendesha kwa manufaa.

 “Bado tunaendelea kuboresha uongozi katika ngazi ya Wakurugenzi ili kuhakikisha kuwa nafasi zote zinazokaimiwa ziweze kujazwa katika ukamilifu wake. ” alibainisha Balozi Muganda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mpya wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Deusdedith Magala ameishukuru Bodi ya STAMICO kwa uteuzi huo na ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu, kujituma na kutoa ushirikiano ili kuhakikisha Shirika linasonga mbele.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bw. Hamisi Komba (aliyeketi kulia) akizungumza na Wakurugenzi (walioketi pamoja) mara baada ya kuripoti katika ofisi ya Kiongozi Mtendaji Mkuu huyo baada ya kuidhinishwa kazini na kuteuliwa kushika nyadhifa mpya. Bw. Deudedith Magala (aliyeketi kushoto) amethibitishwa na Bodi ya STAMICO kuwa Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, nafasi aliyoikaiumkwa miaka mitatu. Aidha Bw. Aloyce Tesha (aliyeketi katikati) ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji na Masoko.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bw. Hamisi Komba (aliyeketi kulia) akizungumza na Wakurugenzi (walioketi pamoja) mara baada ya kuripoti katika ofisi ya Kiongozi Mtendaji Mkuu huyo baada ya kuidhinishwa kazini na kuteuliwa kushika nyadhifa mpya. Bw. Deudedith Magala (aliyeketi kushoto) amethibitishwa na Bodi ya STAMICO kuwa Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, nafasi aliyoikaiumkwa miaka mitatu. Aidha Bw. Aloyce Tesha (aliyeketi katikati) ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji na Masoko.

“Tumejipanga kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wafanyakazi kwa sababu mbalimbali; kufanya tathmini ya mali (asset verification) na kufanya ukaguzi wa rasilimali watu (HR audit) katika kampuni tanzu ya STAMICO na kampuni za wabia wetu ili kuhakiki na kuwatambua mali zilizopo na uwepo wa wafanyakazi pia katika sehemu zao za kazi. Pia tutasimamia zaidi mfumo wa upimaji utendaji kazi yaani OPRAS kwa wafanyakazi wa STAMICO ili wafanyakazi waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo” Alifafanua Bw. Magala.

Bw. Magala ambaye pia amefanya kazi katika Ubalozi wa Ireland kwa miaka tisa, amekuwa mtaalam wa rasilimali watu na utawala katika ngazi ya uongozi kwa zaidi ya miaka 10 sasa; na ana uwezo mkubwa katika ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa ikiwemo miradi ya madini.

Aidha ni Bw. Magala ni mtaalam wa masuala ya diplomasia mwenye uwezo wa kushauri na kusimamia miradi ya Kimataifa ya Maendeleo inayotekelezwa nchini.

Naye  Kaimu Mkurugenzi Mteule wa Uwekezaji na Masoko, Bw. Aloyce Tesha ameishukuru Bodi ya STAMICO kuthamini ujuzi na uzoefu wake katika kazi za sekta ya madini, na ameahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kuhakikisha kuwa miradi ya STAMICO inatekelezwa kwa wakati.

“Naanza kazi kwa kuitathimini upya miradi ya STAMICO na kushauri Menejimenti kuweka kipaumbele katika miradi yenye tija na inayolinda maslahi ya nchi, huku nikihuisha  mahitaji ya soko la bidhaa za madini katika kuibua miradi mipya” alibainisha Bw. Tesha.

Amesema ataendeleza dhana ya kushirikisha nguvu kazi ya wataalam wa Shirika ili kuiwezesha miradi kusimamiwa vizuri na kuleta matokeo yanapimika katika kuinua uchumi wa Shirika

Mkurugenzi mpya wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Deusdedith Magala akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mpya wa Uwekezaji na Masoko wakati alipomtembelea ofisini kwake kufahamu mahitaji yake yakiwemo vitendea kazi.

Mkurugenzi mpya wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Deusdedith Magala akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mpya wa Uwekezaji na Masoko wakati alipomtembelea ofisini kwake kufahamu mahitaji yake yakiwemo vitendea kazi.

Aidha amewaomba wana STAMICO kumpa ushirikiano na kuepuka kutanguliza mbele tofauti za kimadaraja katika kutekeleza majukumu yao, hatua ambayo itasaidia kuweza kufikia malengo ya Shirika kwa ufasaa.

Bw. Tesha ni mtaalam wa miamba wa muda mrefu aliyebobea katika sekta ya madini na amewahi kufanya kazi kama Mratibu Mkazi katika miradi ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa dhahabu na Zebaki nchini Tanzania, inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO).

Vile vile alikuwa Msimamizi wa Mradi wa Kuendeleza Sekta ya Madini (Project Technical Officer) wa kwanza ulioleta mageuzi makubwa katika sekta ya madini nchini, ambao ulikuwa ukidhaminiwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania.

Aidha Bw. Tesha ameshawahi kuwa mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Madini (Southen and Eastern African Mineral Centre- SEAMIC) kwa kipindi cha miaka nane.

============================================MWISHO================================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela
Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
S.L.P 4958,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2150029, 
Barua Pepe: info@stamico.co.tz
Tovuti: http://www.stamico.co.tz
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2018 State Mining Corporation. All Rights Reserved.