Home » News and Events » Jitihada za STAMICO zamfurahisha Waziri wa Madini Mhe. Biteko

Jitihada za STAMICO zamfurahisha Waziri wa Madini Mhe. Biteko

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa jitihada zake katika kuendeleza miradi na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko pichani kulia, wakati akitoa nasaha katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la STAMICO uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akitoa nasaha zake katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Pongezi hizo amezitoa katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Wafanyakazi la STAMICO uliofanyika jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 28 Januari 2020.

Akiongea na wajumbe wa Baraza hilo Mh. Biteko amesema STAMICO sasa imeanza kuleta matumaini ya kiutendaji katika kuendeleza miradi ukilinganisha na miaka michache iliyopita.

Ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya viongozi na wafanyakazi katika kufanya maamuzi na kuitaka STAMICO  kuzidisha juhudi katika kuendesha miradi yake kwa mafanikio ili iweze kuwa taasisi ya mfano katika ukusanyaji wa mapato.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko pichani kulia, wakati akitoa nasaha katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la STAMICO uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko pichani kulia, wakati akitoa nasaha katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la STAMICO uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mhe. Waziri Biteko ameiasa STAMICO kuwa makini katika mikataba inayotaka kuingia kwa kuwashirikisha wataalamu wa sheria kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili iweze kuleta tija kwa Taifa. Aidha amewataka wana STAMICO kuwa waadilifu na waaminifu pindi wanaposimamia shughuli mbalimbali za miradi kwa maslahi ya Taifa.

 Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amesema STAMICO inastahili pongezi kwa kuendesha mkutano huu ya Baraza kwa kuwa ndio sehemu pekee ambayo huwakutanisha wafanyakazi katika kufanya maamuzi ya pamoja yenye tija kwa maendeleo ya Shirika.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Shirika Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dr. Venance Mwasse ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema Shirika linajivunia kutoa mchango Serikalini kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuanza kuuza dhahabu yake katika masoko ya ndani ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dr. Venance Mwasse ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza akiwasilisha taarifa na maazimio ya mkutano wa Baraza  la Wafakazi wa STAMICO kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko

Pamoja na hayo Shirika linaendea kutekeleza shughuli za kibiashara za uchorongaji  pamoja na  kuanza kuendeleza kwa ubia  mradi   wa kujenga mtambo wa kusafisha dhahabu mjini Mwanza.

Kwa upande wa chama cha wafanyakazi (TAMICO) Bw. Samwel Nyungwa, Kaimu Katibu TAMICO Taifa amesema amefurahishwa sana kuona Baraza la Wafanyakazi la STAMICO liko huru katika kutoa maoni na mapendekezo kwa menejimenti na kupokelewa katika mlengo chanya.

Hii ni hatua nzuri ya kiutendaji kwa kuwa inaleta maelewano baina ya uongozi na wafanyakazi na kuepusha migogoro katika eneo la kazi inayoweza kurudisha nyuma jitihada za Shirika.

Kwa upande wa wafanyakazi Bw. Denis Silas ambaye ni Mwenyekiti   wa Chama cha wafanyakazi TAMICO tawi la STAMICO amesema mkutano huu umetoa nafasi ya kutoa maoni yenye lengo la kuboresha miradi na kuongeza tija kwa Shirika na Taifa na kuwa wapo tayari kushirikiana na uongozi ili kutimiza malengo yaliyo katika Mpango Mkakati wa Shirika.

STAMICO imeendelea kufanya Mikutano ya Baraza la Wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ikiwa ni sehemu ya kuwaleta pamoja viongozi na wafanyakazi katika kufanya maamuzi shirikishi yatakayoleta tija kwa Shirika na Taifa kwa ujumla.

————————————————MWISHO——————————————————

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.