Home » News and Events » Mawaziri wavutiwa na Banda la STAMICO kwenye maonesho ya Nanenane

Mawaziri wavutiwa na Banda la STAMICO kwenye maonesho ya Nanenane

Waziri wa Nishati na Madini (W-NM) Mhe. Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (WN OR-TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene kwa nyakati tofauti wametembelea na kuvutiwa na Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. S. Muhongo kushoto, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Mhe. William Tate Ole Nasha katikati na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Idara kuu ya Kilimo Dkt. Laurans Turuka walipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Kuvutiwa kwa Mawaziri hao kunatokana na namna ambavyo Banda la STAMICO na washiriki wake  (Exhibitors)  walivyojipanga katika kutoa maelezo, ufafanuzi na huduma kwa wananchi wanaotembelea Banda hilo sambamba na maonesho maalumu kwa vitendo wanayoonesha kuhusu maswala ya usalama na uokoaji migodini.

Mawaziri hao kabla ya kuoneshwa onesho maalum la namna Mgodi wa STAMIGOLD unavyozingatia swala la usalama na uokoaji mgodini, awali walipatiwa maelezo mafupi kuhusu majukumu ya Shirika la Madini la Taifa na kueleza lengo la kushiriki  kwao katika maonesho  hayo.

Waziri wa Nishati na Madini akiambatana na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Laurans Turuka akiwa kwenye Banda la STAMICO aliwaomba viongozi wa Wizara hiyo kuendelea kuialika STAMICO kila mwaka wakati wa maonesho hayo baada ya kuvutiwa na maelezo waliyopewa Bandani hapo na umuhimu wa Wizara ya Nishati na Madini katika kuchochea uchumi wa nchi.

Nae WN-OR-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mtwara aliipongeza STAMICO na STAMIGOLD kwa jitahada wanazozifanya hasa baada ya kuambiwa kuwa gharama za uendeshaji wa kila siku kwenye Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo zimepungua kwa lengo la kutafuta faida ya shughuli  zinazofanyika mgodini hapo.

Waziri  Simbachawene amewahi kuwa kwenye Wizara ya Nishati na Madini mara mbili kwa nyakati tofauti akiwa kama Naibu Waziri na baadae Waziri kamili, na kwamba majukumu mengi ya STAMICO na STAMIGOLD anayafahamu kwa undani, alifurahishwa na maelezo aliyopewa hali kadharika onyesho maalum la usalama na uokoaji linalolenga kutoa elimu ya usalama na uokoaji migodini.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA KWENYE MAONESHO YA NANENANE  VIWANJA VYA NGONGO LINDI.

Afisa Uhusiano wa STAMICO Bw. Issa Mtuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu majukumu ya Shirika la Madini la Taifa kwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. S. Muhongo alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Afisa Uhusiano wa STAMICO Bw. Issa Mtuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu majukumu ya Shirika la Madini la Taifa kwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Bw. Francis Mng'ong'o Mrakibu kikosi cha Uokoaji mgodini akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini namna wanavyo muokoa mtu mara anapopatwa na tatizo hasa kuzimia akiwa mgodini.

Bw. Francis Mng’ong’o Mrakibu kikosi cha Uokoaji mgodi wa STAMIGOLD mwenye vazi maalum akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini namna wanavyo muokoa mtu mara anapopatwa na tatizo hasa kuzimia akiwa mgodini.

 Kikosi  cha Uokoaji cha Mgodi wa STAMIGOLD (Emergency Response Team) wakiwa wanaonesha umairi wao namna wanavyo wahudumia watu wanaopatwa na matatizo wakiwa mgodini. Hili ni onesho maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wachimbaji wa madini wanaotembelea maonyesho ya Nanenane Ngongo Lindi.

Afisa Uhusiano wa STAMICO Bw. Issa Mtuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu majukumu ya Shirika la Madini la Taifa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

 Kikosi  cha Uokoaji cha Mgodi wa STAMIGOLD (Emergency Response Team) wakiwa wanaonesha umairi wao namna wanavyo wahudumia watu wanaopatwa na matatizo wakiwa mgodini. Hili ni onesho maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wachimbaji wa madini wanaotembelea maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi. Onesho linashudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene mwenye suti Nyeusi.

Kikosi cha uokoaji cha Mgodi wa STAMIGOLD (Emergency Response Team) wakiwa wanaonesha umairi wao namna wanavyo wahudumia watu wanaopatwa na matatizo wakiwa mgodini. Hili ni onesho maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wachimbaji wa madini wanaotembelea maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi. Onesho linashudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene mwenye suti Nyeusi.

Team ya Washiriki wa Nanenane (Exhibitors) kutoka STAMICO na STAMIGOLD wakiwa kwenye  Banda la Maonesho Ngongo Lindi..

Team ya Washiriki wa Nanenane (Exhibitors) kutoka STAMICO na STAMIGOLD wakiwa kwenye Banda la Maonesho Ngongo Lindi..

Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye Banda la STAMICO wakiuliza maswali huku wakisikilizwa na kujibiwa na wataalam

Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye Banda la STAMICO wakiuliza maswali huku wakisikilizwa na kujibiwa na wataalam

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. S. Muhongo kushoto, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Mhe. William Tate Ole Nasha katikati na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Idara kuu ya Kilimo Dkt. Laurans Turuka walipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter  Muhongo kushoto, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha katikati na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Idara kuu ya Kilimo Dkt. Laurans Turuka walipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Moja ya kundi la Wanafunzi wakiwa katika Banda la maaonesho la STAMICO Ngongo Lindi

Moja ya kundi la Wanafunzi wakiwa katika Banda la maonesho la STAMICO Ngongo Lindi

Team ya uokozi ya Mgodi wa STAAMIGOLD ikijiandaa na zoezi la onesho maalum la uokoaji ambalo hufanyika mgodini mara mtu anapopatwa na tatizo linalohitaji msaada

Team ya uokozi ya Mgodi wa STAAMIGOLD ikijiandaa na zoezi la onesho maalum la uokoaji ambalo hufanyika mgodini mara mtu anapopatwa na tatizo linalohitaji msaada

Bw. Francis Mng'ong'o Mrakibu kikosi cha Uokoaji mgodini akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene namna wanavyo muokoa mtu akiwa mgodini mara anapopatwa na tatizo linalohitaji msaada.

Bw. Francis Mng’ong’o Mrakibu kikosi cha Uokoaji mgodini akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene namna wanavyo muokoa mtu akiwa mgodini mara anapopatwa na tatizo linalohitaji msaada.

Afisa Uhusiano wa STAMICO Bw. Issa Mtuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu majukumu ya Shirika la Madini la Taifa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Afisa Uhusiano wa STAMICO Bw. Issa Mtuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu majukumu ya Shirika la Madini la Taifa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye Banda la STAMICO wakiuliza maswali huku wakisikilizwa na kujibiwa na wataalam

Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye Banda la STAMICO wakiuliza maswali huku wakisikilizwa na kujibiwa na wataalam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi

Mratibu wa Maaonesho ya Nanenanne kutoka STAMICO Bibiana Ndumbaro akiandaa mazingira kwa ajili ya onesho la elimu ya usalama na uokoaji migodini

Mratibu wa Maaonesho ya Nanenanne kutoka STAMICO Bibiana Ndumbaro akiandaa mazingira kwa ajili ya onesho la elimu ya usalama na uokoaji migodini

=============================

Imeandaliwa na:

Issa Mtuwa
Afisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma,
Shirika la Madini la Taifa,
Plot 417/418, Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga,
S.L.P 4958,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2150029, 
Barua Pepe: info@stamico.co.tz
Tovuti: http://www.stamico.co.tz

Copyright © 2018 State Mining Corporation. All Rights Reserved.