Home » News and Events » Mhandisi Mchwampaka: “Hongereni STAMICO, mmetimiza ahadi ya kuzalisha Makaa ya Mawe Kabulo-Kiwira”

Mhandisi Mchwampaka: “Hongereni STAMICO, mmetimiza ahadi ya kuzalisha Makaa ya Mawe Kabulo-Kiwira”

  • Asema ni mwanzo wenye kutia matumaini kwa Serikali na Wadau
  • Aitaka STAMICO kwenda na kasi ya ushindani katika soko kupitia uzalishaji bora

Kamishna wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini (MEM) Mhandisi Benjamin Mchwampaka amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kutimiza  ahadi yake ya kuanza kuchimba Makaa ya Mawe katika Mgodi wa Kabulo–Kiwira, hatua ambayo itasaidia kukidhi mahitaji ya madini hayo kwa wadau nchini wakiwemo wazalishaji viwandani.

Kaimu Mratibu wa Mradi wa Makaa ya Mawe-Kabulo Mhandisi Alphonce Bikulamchi (wa pili kutoka kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi kwa Kamishna wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini (MEM) Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa tatu kutoka kushoto) alipoutembelea mradi huo hivi karibuni

Mhandisi Mchwampaka ametoa pongezi hizo hivi karibuni (10/05/2017) alipotembelea mradi huo kwa mara ya kwanza kama Kamishna wa Madini nchini, ili kukagua maendeleo ya Mradi huo wa uzalishaji Mkaa ya Mawe wa Kabulo uliopo katika kijiji Kapeta, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Songwe. Mgodi huo ulianza uzalishaji wake tarehe 30/4/2017.

Kamishna wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini (MEM) Mhandisi Benjamin Mchwampaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kabulo. Wa kwanza kushoto kwake ni Kaimu Mratibu wa mradi huo Mhandisi Alphonce Bikulamchi.

Mhandisi Mchwampaka amebainisha kuwa, hatua ya STAMICO kuanza mradi huo bila kujali changamoto zilizopo kama mvua ambayo husababisha uharibifu wa barabara na magari; inadhihirisha uzalendo wa menejimenti na wafanyakazi katika kutekeleza majukumu ya Shirika, huku ikilenga kuleta matokeo chanya yatakayokuza uchumi wa Shirika na Taifa.

Aidha, Kamishna huyo wa Madini nchini ameitaka STAMICO kuendelea kujiboresha katika matumizi ya vifaa vya kisasa vya uchimbaji ili kukuza uzalishaji wa Makaa ya Mawe wenye viwango hatimaye kukidhi mahitaji ya wateja kwa wakati.

Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa nne kutoka kushoto) na wataalamu wa mradi, wakiwa wameshika makaa kuashiria furaha ya matokeo chanya yaliyopatikana kwa STAMICO kuanzisha mradi huo. Kushoto kwa Kamisha ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO Mhandisi Said Mkwawa na kulia kwake ni Kaimu Mneja Mkuu wa Mgodi wa Kiwira Bwana Aswile Mapamba.

“Kamilisheni haraka uchukuaji sampuli na muufanye upimaji wa sampuli kuwa endelevu katika mradi huu, ili mjiridhishe kila wakati na viwango vya mkaa mnaozalisha, na hivyo kuweza kujinadi kwa uhakika katika soko kulingana na mahitaji ya wateja” Alibainisha Mhandisi Mchwampaka

Aidha, Mchwampaka ameiagiza STAMICO kukamilisha ukarabati wa maabara yake iliyoko katika Mgodi wa Kiwira, ili kazi ya kupima viwango vya ubora Makaa vya Mawe, ianze mara moja na kuliwezesha Shirika kukuza wigo wa soko na na kuufanya mradi kuwa endelevu.

Amesema ofisi yake inashirikiana na STAMICO kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kikamilifu na kwamba Wizara (MEM), itahakikisha miradi ya STAMICO inawanufaisha Watanzania kwa njia mbalimbali ikiwemo ajira na michango katika huduma za maendeleo.

Katika hatua nyingine, Mchwampaka ameilekeza Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO kusimamia kwa karibu na kwa umakini mkubwa mikataba yote ya miradi ya ubia baina ya STAMICO na wawekezaji, ili utekelezaji wa miradi hiyo ulete tija kwa Shirika.

“muendelee kutumia  wataalamu wenu kuboresha mikataba ya ubia na muimarishe usimamizi na ufuatiliaji wa karibu katika miradi yenu, ili kuepuka vikwazo vya kimikataba katika utekelezaji wa miradi” alifafanua Kamishna huyo wa Madini.

Kaimu Mratibu wa Mradi wa Makaa ya Mawe-Kabulo Mhandisi Alphonce Bikulamchi (wa kwanza kushoto) akimuonesha Kamishna wa Madini) Mhandisi Benjamin Mchwampaka eneo la mradi la kuhifadhi Makaa ya Mawe yaliyochimbwa.

Naye Mjumbe wa Bodi ya STAMICO Mhandisi Saidi Mkwawa ambaye pia alishiriki katika ziara amemshukuru Kamishna wa Madini kwa kuutembelea Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kabulo na amemuhakikisha kuwa Bodi ya STAMICO haitamwangusha na itahakikisha kuwa Shirika hilo linakuwa na likabuni miradi mbalimbali ya vipaombele huku ikinufaisha wananchi na Taifa.

Awali Kaimu Mratibu Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kabulo Mhandisi Alhponce Bikulamchi amemweleza Kamishna wa Madini kazi ya uchimbaji Makaa ya Mawe inaendelea vizuri na tayari tani 440 zimechimbwa hadi tarehe 10/05/2017, kiwango ambacho kinatarajiwa kuongezeka zaidi, baada ya  kukoma kwa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Songwe.

Mhandisi Bikulamchi amesema lengo la Mradi ni kuchimba tani 200-300 za Makaa ya Mawe kwa siku, ambapo kwa mwezi mradi unatarajia kuchimba tani 6,000 hadi tani 9,000 za Makaa ya Mawe, kwa kuanzia.

PICHA 6

Kaimu Mratibu wa Mradi wa Makaa ya Mawe-Kabulo Mhandisi Alphonce Bikulamchi (wa kwanza kushoto) akimuonesha Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka eneo la ndani ya Mlima wa Kabuloa ambako Makaa ya Mawe yanachimbwa.

“Mradi huu unatekelezwa kupitia leseni zake mbili za uchimbaji mdogo wa madini Primary Mining Licences (PMLs) zilizopo ndani ya leseni ya utafiti ya Kabulo zenye ukubwa wa Hecta 16.52 na mashapo yapatayo tani 241,865 za mashapo ya makaa ya mawe, yaliyoko karibu na uso wa ardhi  na hivyo kuruhusu Uchimbaji wa Mgodi wa Wazi (Open pit mining) kufanyika” alibainisha Mhandisi Bikulamchi.

============================================MWISHO================================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela
Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
S.L.P 4958,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2150029, 
Barua Pepe: info@stamico.co.tz
Tovuti: http://www.stamico.co.tz
 
Copyright © 2018 State Mining Corporation. All Rights Reserved.