Home » News and Events » STAMICO ILIVYONUFAIKA NA MKUTANO WA SADC

STAMICO ILIVYONUFAIKA NA MKUTANO WA SADC

Jungu kuu halikosi ukoko; huu ni msemo wa wahenga (ukimaanisha panapo jambo kuu hapakosi faida). Msemo huu unaoweza kutumika kwa Watanzania wa sasa kuelezea umuhimu wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Tanzania kuanzia tarehe 17-18Agosti 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dares Salaam.

Kupitia Mkutano huu Tanzania imepewa nafasi ya Mwenyekiti ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhiwa nafasi hiyo atakayoutumikia kwa muda wa mwaka mmoja.

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kupokea uenyekiti, Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wanachama wa SADC kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo madini ili kujiimarisha kiuchumi  kuwa  fursa hiyo ipo wazi.Mkutano huu ulipitisha

Maadhimio 38 ikiwemo kuongeza kasi ya uchumi wa viwanda ili kuleta hamasa ya ukuaji sawa na endelevu wa uchumi wenye lengo la kutokomeza umasikini.

Kwa ujumla Mkutano huu umeacha alama isiyofutika na kuleta matumaini mapya katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii nchini ikiwemo Sekta ya Madini tangu ulipoanza na hata baada ya kumalizika, kwa Watanzania na Nchi Wanachama.

Mkutano huu ulitanguliwa na Maonesho ya Wiki ya Maendeleo ya Viwanda ya SADC yaliyoanza tarehe 5 -9 Agosti 2019 na kifuatiwa vikao mbalimbali vya Viongozi wa Serikali za Nchi Wanachama.

Kupitia maonesho haya STAMICO ilipata nafasi ya kutangaza miradi yake mbalimbali inayoitekeleza na kuisimamia. Moja ya miradi hiyo ni Mradi wa Uchimbaji wa Makaa ya Mawe Kabulo-Kiwira ambapo STAMICO ilitumia fursa hiyo kutafuta soko la makaa ya mawe.

Aidha, katika maonesho hayo Wataalam kutoka STAMICO waliweza kutumia nafasi hiyo kubadilishana utaalamu na baadhi ya wageni walioshiriki katika maonesho hayo.

Bw. Silas akibadilishana uzoefu na Bw. H. Ruzvidzo (kulia) Kutoka Zimbamwe

Bw. Silas akibadilishana uzoefu na Bw. H. Ruzvidzo (kulia) Kutoka Zimbamwe

IMG_6165 (1)

Mjiolojia Denis Silas (kushoto) akielezea kuhusu miradi ya STAMICO kwa Bi. Barati Malinga kutoka Shirika la Maendeleo ya Viwanda ( IDC ) Afrika Kusini (kulia)

 

 

Akizungumzia manufaa ya ushiriki wa STAMICO katika maonesho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bi. Nsalu Nzowa Kaimu Meneja wa Uwekezaji na Masoko anasema maonesho hayo yamefungua fursa kwa wataalam wa STAMICO kujifunza kutoka kwa kampuni na taasisi nyingine za madini za ndani na nje ya nchi wanachama wa SADC ambao walikuja kutembelea maonesho hayo ukizingatia nchi nyingi wanachama wa SADC zina rasilimali kubwa za madini.

Bi. Nzowa anaendelea kueleza kuwa, wageni wengi waliotembelea Banda la STAMICO wamevutiwa na jinsi wataalamu walivyojipanga kulielezea Shirika jinsi inavyotekeleza shughuli mbalimbali katika kuendeleza miradi yake ikiwemo makaa ya mawe ambayo yanachimbwa katika Mgodi wa Kabulo-Kiwira.

IMG_6258

IMG_6246

 

 

 

 

 

Mhandisi Alphonce Bikulamchi Meneja wa uchimbaji (kushoto picha ya kwanza) na mjiolojia Denis Silas (kushoto picha ya pili) wakitoa elimu kwa wageni waliotembelea banda la STAMICO.

Mhandisi Alphonce Bikulamchi Meneja wa uchimbaji (kushoto picha ya kwanza) na mjiolojia Denis Silas (kushoto picha ya pili) wakitoa elimu kwa wageni waliotembelea banda la STAMICO.

“…maonesho haya yamefungua milango ya uwekezaji kwa Shirika kwa kuwa tumeweza kukutana na wadau ambao wameonesha nia ya kutaka kufanya kazi kwa pamoja katika shughuli za madini….”alisisitiza Bi. Nzowa.

Aidha, wakati wa maonesho hayo STAMICO imepata fursa ya kutembelewa na wageni mbalimbali baadhi yao ni wataalamu wa madini ambao walitaka kujifunza kutoka kwetu na vilevile walieleza jinsi wanavyofanya shughuli za madini kwa ufanisi.

Naye Mjiolojia Denis Silas kutoka STAMICO anasema Banda la STAMICO limetembelewa na wageni wengi baadhi yao ni wataalamu ambao wameweza kubadilishana uzoefu katika shughuli za madini hasa katika utafiti na miamba.

“Tumepata fursa ya kujifunza kutoka kwao kwa mfano, kuna miamba miningine ambayo hapa Tanzania hatujaipa kipau mbele katika kuwekeza lakini wenzetu wamewekeza na wanapata faida kutokana na hiyo” Anasisitiza Silas.

IMG_6178

Baadhi ya wageni waliotembelea Banda la STAMICO katika Maonesho ya Nne ya Viwanda-SADC

 

IMG_6096

Baadhi ya wageni waliotembelea Banda la STAMICO katika Maonesho ya Nne ya Viwanda-SADC

Maonesho haya hayajaiacha STAMICO hivi hivi bali yametoa fursa ya kutangaza miradi yake ikiwemo makaa ya mawe ya Kiwira-Kabulo, kutafuta wawekezaji na kujifunza teknolojia mpya ili kuweza kuboresha uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika miradi yetu kuanzia utafiti, uchimbaji na uchakataji.

Maonesho haya ya Nne ya Wiki ya Viwanda-SADC yamelenga kutengeneza mazingira bora ili kuleta maendeleo jumuishi ya viwanda na kutengeneza ajira kwa nchi wanachama za SADC. Maonesho yamekwenda sambamba na mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.

SADC ni Jumuiya yenye historia na mafanikio makubwa Barani Afrika iliyoanza rasmi Agosti 17 1992 kupitia Mkataba uliosainiwa na Wakuu wa Nchi kumi na moja Tanzania ikiwemo. Chimbuko lake lilianza miaka ya 1970 wakati viongozi wa nchi huru wa kiafrika na Vyama vya Ukombozi waliposhirikiana katika masuala ya siasa diplomasia na ukombozi wa waafrika.

 

========================================MWISHO==============================================

Imeandaliwa na:
Afisa Uhusiano,
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
S.L.P 4958,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2150029,
Barua Pepe: info@stamico.co.tz
Tovuti: http://www.stamico.co.tz

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.