Home » News and Events » STAMICO YAKUTANA NA WADAU WA MADINI SABASABA

STAMICO YAKUTANA NA WADAU WA MADINI SABASABA

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limekutana na kujadiliana na Wadau wa Madini katika Mkutano wa Biashara uliofanyika katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa – Sabasaba viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 8/7/2019

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na mwenyekiti wa bodi ya STAMICO Meja Generali mstaafu Michael Isamuyo mara baada ya kufungua Mkutano wa Biashara wa Wadau wa Madini

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na mwenyekiti wa bodi ya STAMICO Meja Generali mstaafu Michael Isamuyo mara baada ya kufungua Mkutano wa Biashara wa Wadau wa Madini

 

Mkutano huo umefunguliwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kutoa rai kwa wadau kutumia nafasi hiyo kujadili fursa na changamoto na kuzitafutia suluhisho.

Naibu Waziri Nyongo amezitaka Taasisi za Serikali kupokea ushauri, maoni na mapendekezo yatakayotolewa na wadau ili kupata njia bora ya kutatua changamoto hizo.

Aidha aliitaka TANTRADE kuendelea kuwakutanisha wadau wa madini wa ndani na nje ya nchi ili waweze kubadilishana maarifa, uzoefu na teknolojia katika shughuli za madini.

Kwa upande wa STAMICO Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Generali mstaafu Michael Isamuyo amesema mkutano huu umefungua milango kwa STAMICO kukutana na wadau wa madini ili kuboresha sekta hii na kuchangia pato la taifa.

 

Wadau mbalimbali waliotembelea banda la STAMICO wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa – Sabasaba 2019

Wadau mbalimbali waliotembelea banda la STAMICO wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa – Sabasaba 2019

Isamuyo amesema ushirikiano uliopo baina STAMICO na TANTRADE utaleta mabadiliko makubwa katika soko la madini na teknolojia kwa wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakitumia teknolojia duni.

Akiongea kwa niaba ya wachimbaji wadogo Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo Bw. John Bina amewaomba wachimbaji wadogo na wadau wa madini kutumia fursa hizi za mikutano ya kibiashara kutoa changamoto na njia ya kuzitatua kwa manufaa yao na Serikali.

Ameiomba TANTRADE kuratibu mikutano hii ya madini katika mikoa mbalimbali ili iweze  kuwafikia wananchi wote Zaidi ya hapa Dar es Salaam.

STAMICO imeshiriki katika Mkutano wa Biashara uliofanyika tarehe 8/7/2019 katika maonesho ya Biashara ya kimataifa – Sabasaba yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, mkutano huu umelenga kuwakutanisha wadau wa madini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na umeshirikisha Tume ya Madini, Tantrade, STAMICO, Wachimbaji Wadogo na Wafanyabiashara wa Madini.

 

========================================MWISHO==============================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela

Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.