Home » News and Events » STAMICO yapata mafunzo ya Zimamoto

STAMICO yapata mafunzo ya Zimamoto

Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wamepewa mafunzo ya kuzima moto pindi wanapokutana na janga la moto wawapo kazini na katika maeneo yao ya kuishi.

Mafunzo haya yametolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na askari wa Jeshi la Zima Moto kutoka jijini Dar es Salaam.

1

1b

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mha. Kanali Sylvester Ghuliku (pichani kushoto) akifungua mafunzo ya kuzima moto yaliofanyika STAMICO Makao Makuu. Picha ya kulia ni wafanyakazi wakiwa katika mafunzo hayo

 Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mha. Sylvester Ghuliku amewaasa wana STAMICO kuacha kutaharuki pindi moto unapotokea na badala yake kutulia na kuukabili moto ili kuepuka athari kubwa zinazoweza kutokea.

 “Moto ukiudhibiti mapema unaweza kuzimwa kwa bilauri moja ya maji”, alisisitiza Kanali Ghuliku huku akiwataka wafanyakazi wote kufuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyotolewa kwa nadharia na vitendo.

2

Kamanda Yusto Mlay kutoka Jeshi la Zima Moto (wa kwanza kulia) akiwasisitizia wana STAMICO kutumia vifaa vinavyotakiwa katika  kuzima moto

 Naye mwezeshaji kutoka Jeshi la Zima Moto Kamanda Yusto Mlay amesema ni vyema watu watambue visababishi  vya moto na kujua namna ya kuudhibiti kulingana na vyanzo vyake ili kuwezesha udhibiti wa moto huo kwa haraka.

3

 Kaimu Meneja Rasilimali Watu wa STAMICO Bw. Lameck Kabeho (aliyeshika kifaa cha kuzimia moto) akizima moto kwa vitendo mara baada ya mafunzo

Kamanda Mlay amewataka wafanyakazi wa STAMICO kutopuuzia kujiwekea mazoea ya kununua vifaa vya kitaalamu vya kuzima moto katika ofisi, vyombo vyao vya usafiri na makazi binafsi ili  kujijengea uwezo wa kudhibiti moto pindi unapotokea.

4 5

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 Wafanyakazi wa STAMICO wakifanya mazoezi ya kuzima moto kwa vitendo baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mkufunzi. Pichani juu kushoto ni Bi Misky Massawe Mhasibu wa STAMICO akiwa katika zoezi la kuzima moto na pichani juu kulia ni Bw. Hamis Mdoe Msaidizi wa Kumbukumbu-STAMICO akishiriki zoezi la uzimaji moto 

Aidha Mkufunzi huyo alitoa mafunzo ya kuzima moto kwa njia za asili ili kuwawezesha wafanyakazi kuudhibiti moto ukiwa katika hatua za mwanzo endapo utatokea wakati wakisubiri msaada kutoka Jeshi la Zima Moto.

 Akitoa shukrani kwa uongozi wa STAMICO Bw. Hamis Mdoe kwa niaba ya wafanyakazi wote amesema mafunzo hayo yamefungua mwanga kuhusu kudhibiti moto na kuwezesha kujua vifaa mbalimbali vya kuzima moto ikiwemo vya asili na vya kisasa.

 STAMICO imeendelea kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake katika taaluma mbalimbali zaidi ya na mafunzo ya zima moto. Mafunzo ya kuzima yalitolewa ili kuwajengea wafanyakazi uwezo wa kukabiliana na moto katika hatua za awali hatimaye kupunguza madhara yatokanayo na moto sehemu za kazi na hata katika makazi yao binafsi.

==============================MWISHO=============================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela

Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2019 State Mining Corporation. All Rights Reserved.