Home » News and Events » STAMICO YATOA ELIMU YA MIAMBA

STAMICO YATOA ELIMU YA MIAMBA

Shirika la madini la taifa limeendelea kutoa elimu kuhusu miamba ya madini inayopatikana nchini kwa wananchi mbalimbali waliokuja kutembelea banda wakati wa Maonesho ya Kibiashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam

Mjiologia wa STAMIGOLD  Gwalugano Mwamalala akitoa elimu ya miamba kwa wadau waliotembelea banda la STAMICO.

Mjiologia wa STAMIGOLD Gwalugano Mwamalala akitoa elimu ya miamba kwa wadau waliotembelea banda la STAMICO.

Akiongea  kuhusu miamba mjiologia kutoka Stamigold Bw. Gwalugano Mwamalala amesema watu wengi wanaotembelea banda la STAMICO wana uelewa mdogo kuhusu miamba ukilinganisha na wale wanaoifahamu hivyo wanatumia muda kuwaelimisha,

Baadhi ya wadau wakiangalia miamba kwa ktumia kifaa maalumu ili  kuweza kubaini aina ya madini yaliyopo katika miamba hiyo

Baadhi ya wadau wakiangalia miamba kwa ktumia kifaa maalumu ili kuweza kubaini aina ya madini yaliyopo katika miamba hiyo

Mwamalala amesema elimu inatolewa kulingana na mahitaji ya watu kwani kumekuwa na ugumu katika kuwaelimisha kutokana na taarifa za awali walizonazo kuhusu miamba na madini

‘Inachukua muda mrefu kuwaelimisha na kukubaliana na maelezo ya wataalamu hasa katika matumizi ya vifaa vya kupimia miamba hususani dhahabu (metal detactor).

IMG_5407

Baadhi ya wananchi wameonesha kufurahishwa sana na elimu inayotolewa kwa kuwa wengi wao wamekiri kufahamu kwa nadharia wakati wakiisoma darasani bila kuona kiuhalisia hivyo kushindwa kutofautisha kwa usahihi aina za miamba mbalimbali.

Wameipongeza STAMICO pamoja  na kampuni yake tanzu ya STAMIGOD Biharamulo Mine kwa kuleta wataalamu wa miamba (wajiolojia) ambao wanatoa elimu kwa vitendo na kuonesha sampuli za miamba ya madini

“Leo STAMICO mmenisaidia kuondoa utata katika kutofautisha miamba . Elimu hii imenifungua kwani nilikuwa nashindwa kuwana ujasiri  wa kusimama mbele ya wanafunzi ambao walishaaminishwa kuwa  majiolojia ndio pekee wanaweza itofautisha miamba kwa uhakika Alisema Bw, Fortnatus.

STAMICO imeendelea kupokea wageni mbalimbali wanaokuja kujifunza kuhusu madini na shughuli zinazofanywa na Shirika hilo ili kupunguza na kuondoa sintofahamu zilizopo katika miamba ya madini.

 

 

 

 

========================================MWISHO==============================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela

Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

 

 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.