Home » News and Events » STAMIGOLD YATOA ELIMU YA UOKOAJI MIGODINI

STAMIGOLD YATOA ELIMU YA UOKOAJI MIGODINI

Kampuni tanzu ya STAMICO, STAMIGOLD Biharamulo Mine imetoa  elimu ya uokoaji katika migodi na mazingira yanayoizunguka

Elimu hiyo imetolewa kwa vitendo na wataalamu wa mazingira wakati wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa- Sabasaba yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

Afisa Usalama na Afya za Wafanyakazi –STAMIGOLD akiwaelezea wadau shughuli za usalama zinazofanyika katika mgodi wa STAMIGOLD

Afisa Usalama na Afya za Wafanyakazi –STAMIGOLD akiwaelezea wadau shughuli za usalama zinazofanyika katika mgodi wa STAMIGOLD

Akiongea kuhusu ushiriki wao katika maonesho Bw. Fred Makwebeta Afisa Usalama na Afya za Wafanyakazi kutoka STAMIGOLD amesema, tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi,mazingira na viumbe hai kwa ujumla hivyo tumeamua kuleta elimu ya kujikinga na athari zinazoweza kusababisha kuumia na hata kupelekea vifo.

Elimu ya uokoji ni muhimu kwa watu mbalimbali hususani wanaoishi katika maeneo ya migodi ili waweze kujikinga na athari zinazoweza kuwapata kutokana na shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini.

Wadau wakiangalia vifaa vya uokoaji migodini wakati maonesho

Wadau wakiangalia vifaa vya uokoaji migodini wakati maonesho

Tumeamua kuileta elimu hii katika viwanja vya sabasaba kuweza kuwafikia wadau wengi wa madini ili kuwajengea uwezo wa kutoa msaada na kujisaidia wenyewe pale inapohitajika. Na tunaahidi kuendelea kuwafikia wananchi wengi Zaidi.

Wadau wakiangalia vifaa vya uokoaji migodini wakati maonesho.

Wadau wakiangalia vifaa vya uokoaji migodini wakati maonesho.

Kampuni ya STAMIGOLD imetumia  Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kukutana na wadau na pia imeleta vifaa vya uokoaji ili watu waweze kuviona kwa macho, wajifunze na kujua matumizi yake.

 

 

========================================MWISHO==============================================

Imeandaliwa na:

Bibiana Ndumbaro

Afisa Uhusiano,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.