Home » Events » UBUNIFU ULIOTUKUKA NGUZO KUU YA MAFANIKIO STAMICO-MHANDISI NAYOPA

UBUNIFU ULIOTUKUKA NGUZO KUU YA MAFANIKIO STAMICO-MHANDISI NAYOPA

Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wametakiwa kutumia ubunifu uliotukuka katika kutekeleza miradi ya Shirika hususani wakati huu ambapo Shirika hilo linajitathimini kuboresha utendaji kazi wake ili kuleta matokeo chanya yatakayoinua ukuaji wa uchumi nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa ametoa wito huo hivi Karibuni alipokutana na Wafanyakazi, kupokea kwa mipango kazi ya Kurugenzi, Idara na Vitengo ambayo imeboreshwa ili kwenda sambamba na dhana ya kujitathimini upya kwa Shirika hilo na kujiendesha Kibiashara.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa (Mwenye Koti la Brown) akiwasisitiza Wafanyakazi kutumia ubunifu uliotukuka kama nguzo ya kuleta maendeleo ya Shirika. Mhandisi Nayopa alisisitiza hayo, katika kikao chake na Wafanyakazi kilicholenga kupokea kwa pamoja mipango kazi ya kuimarisha utendaji na kuliwezesha Shirika kujiendesha Kibiashara.

“Kama Kiongozi Mtendaji Mkuu wa STAMICO, nitahakikisha Mipango Kazi hii inashuka kwa kila mtumishi na kuwezesha kila mmoja wetu kuwa na mpango kazi wake wa siku, wiki, mwezi, robo mwaka na hata mwaka; hatua ambayo itarahisisha upimaji wa matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu yetu” Alisisitiza Mhandisi Nayopa.

Amesema mipango kazi hiyo iliyoboreshwa  ni matokeo ya andiko la tafakari ya jinsi STAMICO tunavyokusudia kusonga mbele katika  kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kulifkisha kuinua kiwango cha Shirika cha kiwango cha uzalishaji bidhaa za madini na hivyo kuunga mkono kwa vitendo dhima ya Serikali ya awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.

Andiko hilo la kujitathimini limewasilishwa Wizara ya Madini ili kuishirikisha Wizara katika kutatua changamoto husika hatimaye kuiwezesha STAMICO kutekeleza miradi yake kikamilifu ikiwemo ile ya kuwaendeleza wachimbaji.

“Ndugu Wafanyakazi napenda mtambue kuwa miradi yetu vipaombele kwa sasa ni Kiwira, Buhemba, Mradi wa uzalishaji Kokoto na Miradi ya Ubia. Ili tuweze kufikia mabadiliko tunayotarajiwa kufanya katika miradi hii, ni lazima Menejimenti na Watumishi tukubali kwa pamoja kubadilika. Hi itatuwezesha kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa miradi hatimaye kutokomeza ulemavu uliokuwepo awali” Alibainisha Mhandisi Nayopa.

Aidha, Mhandisi Nayopa amewataka Wafanyakazi wa STAMICO kuacha kufanya kazi kwa mazoea na katika standards za chini, bali wajikite zaidi kuinua viwango vyao vya uwajibikaji na kuhuisha matumizi sahihi ya teknolojia za kisasa katika kutekeleza majukumu yao.

Hivi karibuni, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko alitembelea ofisi za STAMICO Makao Makuu zilizopo jijini Dar es Slaa ambapo Ofisi alikutana na Menejimenti na Wafanyakazi wa Shirika hilo na kuwaagiza kujitathimini upya ili kuboresha utendaji kazi wake na kuleta matokeo yenye manufaa kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao Menejimenti na Wafanyakazi wa STAMICO wamemuhakikishia Mhandisi Nayopa kuwa wamejipanga upya na watakuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo; ambapo pia walikiri mapungufu yao na kuazimia kubaini changamoto zinazojitokeza sehemu ya kazi na kuzitatua kwa wakati, ilikufikia malengo yaliyokusudiwa.

Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya STAMICO na Wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wao, Mhandisi John Nayopa (picha iliyotangulia mwanzo wa habari hii) katika kikao cha kuwasilisha mipango kazi yao inayolenga kuimarisha utendaji na kuliwezesha Shirika kujiendesha Kibiashara.

Mhandisi Nayopa pia alitumia kikao hicho kuwataarifu Wafanyakazi kuwa ameunda Timu ya Mabadiliko (Change Agent Team) yenye wajumbe wawili kwa kuanzia, wataofuatilia utekelezaji wa majukumu ya Shirika kwa kila mtumishi kila siku ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wakati uliopangwa.

Katika Mkutano huo, Wafanyakazi walipata fursa ya kutoa maoni yao namna watakavyotekeleza kikamilifu dhima ya Hapa kazi tu katika Kurugenzi, Idara na Vitengo vyao ili kufikia malengo ya kuliendesha Shirika Kibiashara.

Msaidizi wa Ofisi wa STAMICO ambaye pia ni Naibu Katibu wa Tawi la TAMICO-STAMICO Bwana Mohamed Kaunya akichangia jambo katika kikao cha Wafanyakazi kilicholenga kupokea mipango kazi ya kuimarisha utendaji na kuliwezesha Shirika kujiendesha Kibiashara

Mtunza Kumbukumbu na Nyaraka wa STAMICO Bwana Hamisi Mdoe akitoa maoni yake kuhusu umuhimu wa Mashirika ya Umma kutoa kipaumbele katika kulipa madeni yakiwemo ya Wafanyakazi, ili kudumisha morali yao katika kazi

STAMICO ni Shirika linalomilikiwa na Serikali na lilianzishwa rasmi mwaka 1972 ili kusimamia maslahi ya Taifa katika Sekta ya Madini, kwa niaba ya Serikali.

Shirika hilo lilifanyiwa marekebisho kupitia Hati ya Kurekebisha Uanzishwaji wa STAMICO (The Public Corporation State Mining Corporation Establishment Amendment Order, 2015) mnamo tarehe 5 Machi, 2015.

Kwa hati hiyo, STAMICO iligeuzwa rasmi kuwa chombo cha kusimamia maslahi ya Serikali katika rasilimali za madini pamoja na kuwekeza katika Miradi ya Kimkakati  ili kuongeza manufaa ya madini katika Pato la Taifa.

5

==============================MWISHO=============================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela

Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

Copyright © 2019 State Mining Corporation. All Rights Reserved.