USHIRIKI KATIKA MAONESHO YA VIWANDA YA SADC
Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) limeshiriki katika maonesho ya viwanda ya Jumui ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwaafrika yanayo fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Maonesho haya yenyekauli mbiu “Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya Jumuiya” yamefunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli Agasti 5, na kutarajiwa kuisha Agasti 8, 2019.
STAMICO imeshiriki ili kujitangaza na kutafuta wawekezaji ikiwemo wanunuzi wa makaa ya mawe ambayo yanachimbwa katika Mgodi wa Kabulo katika mkoa wa Songwe.
Maonesho haya yanafungua milango kwa wawekezaji kuweza kujifunza na kujadiliana kuhusu sualanzima la uwekezaji katika sekta ya madini.
Aidha kupitia maonesho haya STAMICO inatafuta wawekezaji ambao tunaweza kuingia nao ubia katika baadhi ya miradi ya STAMICO.
========================================MWISHO==============================================
Imeandaliwa na:
Bibiana Ndumbaro
Afisa Uhusiano,
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
S.L.P 4958,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2150029,
Barua Pepe: info@stamico.co.tz
Tovuti: http://www.stamico.co.tz