Home » News and Events » Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini kuepukana na uchimbaji wa kubahatisha

Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini kuepukana na uchimbaji wa kubahatisha

Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) imenunua Mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba wenye thamani ya Dola za Kimarekani 1,378,654.48  kwa ajili ya uchorongaji wa bei nafuu kwa  Wachimbaji wadogo ili usaidie wachimbaji hao nchini kuondokana na uchimbaji duni wa kubahatisha kwani kwa kutumia mtambo huu wataweza kupata taarifa za mashapo kwa haraka zaidi zitakazo wapa uhakika wa kupata madini sehemu wanayochimba.

Wataalam wa Uchorongaji na Utafiti wa Madini (Drillers & Geologist) wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuendesha (operate) mtambo wa kisasa wa uchorongaji (multi-purpose air rotary drill rig) Kushoto pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji miamba Bw. Alex Rutagwelela kutoka STAMICO

Wataalam wa Uchorongaji na Utafiti wa Madini (Drillers & Geologist) wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuendesha (operate) mtambo wa kisasa wa uchorongaji (multi-purpose air rotary drill rig) Kushoto pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji miamba Bw. Alex Rutagwelela kutoka STAMICO

Ujio wa Mtambo wa Uchorongaji miamba unaojulikana kama “multi-purpose air rotary drill rig”  wenye uwezo wa kufanya kazi za uchorongaji wa miamba wa aina tatu: Reverse Circulation (RC) hadi mita 200, Rotary Air Blast (RAB) hadi mita 150 na NQ Air Core hadi mita 30 ni mkombozi kwa wachimbaji wadogo,na  wakati nchini na utasaidia ili  kuachana na uchimbaji wa kubahatisha kama ilivyo sasa.Aidha wawekezaji wakubwa wa utafiti na uchimbaji madini wanayo nafasi pia ya kutumia mtambo huu kwa gharama nafuu.

Akiongea wakati wa mafunzo ya siku tano namna ya kuendesha mtambo huo kwa wataalam wa Jiolojia na Uchorongaji wapatao 16 kutoka taasisi tano zilizo chini ya wizara ya Madini (STAMICO, GST, MRI, Tume ya Madini na Ofisi ya Kamishina wa Madini) Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji Bw. Alex Rutagwelela ambae ni mtaalam na mbobezi katika masuala ya uchorongaji kutoka  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) amesema mtambo huo ni wa kisasa na unauwezo mkubwa wa kufanya kazi tofauti tofauti ambazo zingefanywa na mitambo mitatu tofauti lakini sasa zinawez kufanyika kwa kutumia mtambo huo huo mmoja na ndio maana unaitwa “multi-purpose air rotary drill rig”.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ofisi za STAMICO Dodoma kuanzia tarehe 03- 07/12/2018 ili kuwajengea uwezo wataalam hao namna ya kuendesha (operation procedures) mtambo huo kabla ya kuanza kututumika.

“Mafunzo haya ni muhimu sana kwa wataalam wetu hususan wajiolojia,wahandisi mitambo na wachorongaji miamba kwani Mtambo huu (multi-purpose air rotary drill rig”.) una aina nyingi za mfupo wa uchorongaji wa kutumia upepotofauti na mfumo wa uchorongaji wa aina ya Diamond (DD). Kutokana na  hali hiyo Wizara ya Madini kupitia mradi wa SMMRP kwa kushirikiana na STAMICO tuliona umuhimu wa kutoa mafunzo haya kwa wataalam wetu ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuutumia na kuutunza mtambo huo”. Alisema Bw. Rutagwelela.

Bw.Rume Laghati.. kushoto, kutoka Geofield Drilling Company Ltd mtaalam wa uchorongaji miamba akimuelekeza kwa vitendo Bw. Mshaka Mdeke kutoka STAMICO namna mbalimbali ya ku-operate mtambo wa uchorongaji miamba aina ya “multi-purpose air rotary drill rig”.

Bw.Rume Laghati (kushoto) kutoka Geofield Drilling Company Ltd mtaalam wa uchorongaji miamba akimuelekeza kwa vitendo Bw. Mshaka Mdeke kutoka STAMICO namna mbalimbali ya ku-operate mtambo wa uchorongaji miamba aina ya “multi-purpose air rotary drill rig”.

Wataalam waliopewa mafunzo hayo akiwemo Mha. Benard Nsiyani na Mashaka Mdeke wamesema wamefurahia mafunzo hayo kwani wamejifunza mengi., Kwa upande wake Bw. Mdeke  ambaye ni mtaalam wa kuchoronga miamba alimwambia mwandishi wa habar hizi kuwa alizoea kuchoronga kwa kutumia “DD hivyo kupewa mafunzo ya mtambo ambao ni “multi-purpose air rotary drill rig”  yamemuongezea ujuzi.

Bw. Rume Laghati kutoka Geofield Drilling Company Ltd mtaalam wa uchorongaji miamba aliyekuwa mwezeshaji wa mafunzo hayo alisema maamuzi ya Wizara kuwapa mafunzo wataalam hao ya namna ya kuendesha mtambo huo ulikuwa sahihi kwa kuwa namna uendeshaji wa mtambo huu (operation standard procedures) ni tofauti na mitambo mingine, kwani kwenye mtambo huu ni wa kisasa zaidi na una  mambo ya ziada  tofauti na mitambo mingine.

AC6A0065

Wataalam wa Uchorongaji na Utafiti wa Madini wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuendesha (operate) mtambo huo wa kisasa wa uchorongaji

Mtambo huo ulionunuliwa na Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) kwa thamani ya Dola za Marekani 1,378,654.48 ni mahususi kwa ajili ya kuwezesha tafiti za kina za kijiolojia zenye lengo la kufanya ukadiriaji na uthamini wa mashapo ya madini katika maeneo mbali mbali ya nchi na hususan maeneo ya wachimbaji wadogo ili uwasaidie kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha na kuhusisha ushirikina.

Bw. Rutagwelela akiongea  kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO ameishukuru Wizara ya Madini na Mradi wa SMMRP kwa kufanikisha upatikanaji wa mtambo huo kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Ametoa wito kwa wachimbaji wadogo kuchangamkia fursa ya hiyo kwa kuutumia mtambo huo  wa gharama ndogo za uchorongaji katika uchimbaji wao.

================================== MWISHO =============================

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.