Home » Breaking News » Waziri Mkuu Majaliwa afurahishwa na utendaji kazi wa STAMICO

Waziri Mkuu Majaliwa afurahishwa na utendaji kazi wa STAMICO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya  Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa amepongeza shughuli za Shirika za uwekezaji katika sekta ya Madini Nchini.

Pongezi hizo amezitoa alipotembelea maonesho ya yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Tanzania wa Mwaka 2020 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa akiwa ameambatana na Waziri wa Madini Mhe. Biteko wakipata maelezo ya utendaji kazi wa STAMICO kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Dr. Venance Mwasse

Akielezea shughuli za shirika,  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa   STAMICO Dk Venance Mwasse  alieleza kwamba.Shirika linaendelea vizuri  na shughuli zake za uwekezaji pamoja na changamoto inazopitia. “Shirika  limejipanga kuendeleza miradi yake ikiwa ni pamoja  na  kuongeza  mashine za chorongaji  ili kukidhi mahitaji ya wateja ” alieleza Dk Mwasse.

Pia  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji aliongeza kuwa   kwa sasa  mgodi wa STAMIGOLD  unaendeshwa kwa faida  na  umepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji. Mgodi wa STAMIGOLD  unamilkiwa na STAMICO  na unaendeshwa na wazawa kwa asilimia 100.

Katika mkutano huu Mheshimiwa Majaliwa pia alizindua hati ya uhalisia ya Madini ya bati ambayo itaiwezesha Tanzania kuuza Madini ya Bati popote duniani.

—————————————————————————————————-

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.