Home » News and Events » WAZIRI WA MADINI AWATEMBELEA STAMICO – SABASABA

WAZIRI WA MADINI AWATEMBELEA STAMICO – SABASABA

Waziri wa Madini Dotto Biteko (Mb) atembelea Banda la STAMICO leo 12/07/2019 katika maonesho ya biashara ya kimataifa- sabasaba yanaendelea viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Waziri wa Madini Dotto Biteko (Mb) akiangalia sampuli za miamba ya madini alipotembelea banda la STAMICO (kushoto) kulia nia Mjiolojia  Denis Silas- STAMICO

Waziri wa Madini Dotto Biteko (Mb) akiangalia sampuli za miamba ya madini alipotembelea banda la STAMICO (kushoto) kulia nia Mjiolojia Denis Silas- STAMICO.

Waziri Biteko Ameipongeza STAMICO pamoja na kampuni ya yake tanzu ya STAMIGOLD kwa kushiriki katika maonesho na kuitaka kuzidi kuongeza juhudi ya utendaji kazi katika miradi yake.
Aidha viongozi mbalimbali nao watembelea banda la STAMICO wakati wa maonesho akiwemo Ndugu Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara), Prof. Idris Kikula Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Ndugu Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara) akiambatana na Mkurugenzi mkuu wa Tantrade bw. Edwin Lutagweruka.
Kwa upande mwingine STAMICO ilitembelewa na Dr. Athanas Macheyeki Kamishna wa Tume ya Madini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) Bi. Yokubeth Muyumbilwa, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB bw. Charles Singili.

Ndugu Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara) akipokea maelezo ya miamba ya madini kutoka kwa Mjiolojia wa STAMICO Denis Silas

Ndugu Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara) akipokea maelezo ya miamba ya madini kutoka kwa Mjiolojia wa STAMICO Denis Silas

Prof. Idris Kikula Mwenyekiti wa Tume ya Madini (kulia)akipokea maelezo kuhusu kemikali za uchenjuaji wa dhahabu kutoka kwa Sikini Nyankisinda Mmetalajia wa STAMIGOLD

Prof. Idris Kikula Mwenyekiti wa Tume ya Madini (kulia)akipokea maelezo kuhusu kemikali za uchenjuaji wa dhahabu kutoka kwa Sikini Nyankisinda Mmetalajia wa STAMIGOL

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) Bi. Yokubeth Muyumbilwa (kushoto) akipata maelezo kuhusu vifaa vya uokoaji migodini kulia ni Fred Makwebeta Afisa Usalama na Afya za wafanyakazi-STAMIGOLD.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB bw. Charles Singili akipata maelezo kuhusu vifaa vya uokoaji migodini

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB bw. Charles Singili akipata maelezo kuhusu vifaa vya uokoaji migodini

========================================MWISHO==============================================

Imeandaliwa na:

Bibiana Ndumbaro

Afisa Uhusiano,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

Copyright © 2020 State Mining Corporation. All Rights Reserved.