Home » Events » ZIARA YA WAZIRI WA MADINI YALETA TIJA KWA STAMICO

ZIARA YA WAZIRI WA MADINI YALETA TIJA KWA STAMICO

IMG_9684

IMG_9681

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Ziara ya Waziri wa Madini . Angellah Kairuki (Mb) alioifanya tarehe 05.11.2018 katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), imeleta tija, baada ya Wizara ya Madini kuchangia shilingi milioni 24 ili kuongezea nguvu ya kutekeleza mradi wa Kokoto wa Shirika uliopo eneo la Ubena Zomozi, mkoani Pwani.

Mhe. Kairuki alitoa mchango huo baada ya kuguswa na tatizo la ukosefu wa mitaji ya kutekeleza miradi, kama lilivyobainishwa katika taarifa ya utendaji kazi ya Shirika hilo iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi Sylivester Ghuliku; kwenye kikao cha pamoja baina ya Mhe. Waziri, Wafanyakazi na Katibu Mkuu, Profesa Simon Msanjila na Wafanyakazi.

Fedha hizo zitaiwezesha STAMICO kufikia bajeti yake ya Shilingi milioni 54 baada ya Shirika pia kuchangia Shilingi milioni 30 zinazohitajika kufanya utafiti wa kijiolojia unaolenga kubaini ubora wa mwamba katika eneo la Chigongwe, ambapo awamu ya kwanza ya mradi wa kokoto wa STAMICO itatekelezwa.

Mhe. Kairuki aliwataka Wafanyakazi kukuza ubunifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi, huku akiwataka kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuboresha utendaji kazi wa STAMICO wenye tija kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Maoni hayo yatawasilishwa kwa maandishi na kila mfanyakazi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila; katika kikao maalum kitakachofanyika ofisi za STAMICO ndani ya siku saba kuanzia tarehe 5/11/2018.

2

Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya STAMICO na Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (MB) (hayupo pichani) alipotembelea Shirika la Madini la Taifa, tarehe 5 Novemba 2018 katika ofisi za Makao Makuu ya STAMICO zilizopo barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga jijini Dar es Salaam na kufanya kikao nao

Waziri wa Madini Mhe. Kairuki na Katibu Mkuu wake Prof. Msanjila, wameipongeza STAMICO kwa kuweka Menejimenti mpya katika Kampuni yake tanzu ya STAMIGOLD kwani imesaidia kujiendesha kwa faida, kuimarisha ulipaji madeni na kumudu gharama za uendeshaji mgodi.

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (MB) aliyekaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na Wafanyakazi wa STAMICO baada ya kukamilisha ziara yake katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi Sylvester Ghuliku na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi  Sylvester Ghuliku amemshukuru Mhe. Waziri Kairuki kwa ziara hiyo na ushirikiano anaoutoa kwa STAMICO ili kuhakikisha Shirika linakua kwa kasi na kuleta manufaa mapana kwa Taifa na kwa maendeleo ya Watanzania.

Mhandisi  Kanali Ghuliku ameMheakikishia Mhe. Waziri kuwa STAMICO imedhamiria kuleta mabadiliko katika miradi yake kwa kuboresha miundombinu ya miradi, mifumo ya uangalizi na ufuatiliaji na kupunguza gharama za uendeshaji migodi ili kuongeza faida na tija kwa Taifa.

Akitoa neno la shukrani, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa STAMICO Meja Luyodrey Masaki amesema kikao hicho cha pamoja na Mhe. Waziri kimekuwa kichocheo cha uwajibikaji kama Shirika na kwa mtu mmoja mmoja na amemuahidi Waziri kuwa STAMICO itarekebisha mapungufu yake na kutoa maoni ya maboresho Wizarani, ili kuleta tija kwa Shirika.

Meja Masaki ameishukuru Wizara kwa mchango wake wa Shilingi milioni 24 ambazo zitasadia kutekeleza Mradi wa Kokoto wa Ubena Zomozi, na hivyo kuwezesha kukidhi mahitaji ya kokoto katika miradi ya  mindombinu ya barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege; sambamba na majengo ya biashahara, ofisi na makazi.

Mapema mwezi huu Novemba, Waziri huyo wa Madini ameitembelea STAMICO ikiwa ni ziara yake ya pili kwa mwaka 2018; iliyolenga kufuatilia utendaji kazi wa Shirika, changamoto zake, mbinu za utatuzi wa changamoto na mwelekeo wa uendeshaji Shirika kwa kasi itakayoleta matokeo chanya nchini.

 

==============================MWISHO=============================================

Imeandaliwa na:

Koleta Njelekela

Meneja Masoko na Mawasiliano kwa Umma,

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),

S.L.P 4958,

Dar es Salaam.

Simu: +255-22-2150029, 

Barua Pepe: info@stamico.co.tz

Tovuti: http://www.stamico.co.tz

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Copyright © 2019 State Mining Corporation. All Rights Reserved.