Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

BODI YA SHIRIKA LA MADINI LA TAIFA (STAMICO) YATEMBELEA KITUO CHA MFANO KATENTE


Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), leo tarehe 17/07/2023 imetembelea Kituo cha Mfano kwa wachimbaji wadogo Katente katika ziara yake ya kikazi kukagua maendeleo ya utendaji kazi wa kituo hicho kilichopo Kata ya Katente, wilayani Bukombe.

Akizungumza na watumishi wa kituo hicho pamoja na Menejimenti ya Shirika, Mwenyekiti wa Bodi, Meja Jenerali(Mst) Michael Isamuhyo ameeleza kwamba Bodi imeridhishwa na maendeleo chanya ya kituo hicho. Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Bodi pamoja na wajumbe wake waliwaasa wafanyakazi wa kituo hicho kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuweza kufikia malengo ya kituo hicho ambayo ni kutoa elimu ya vitendo kwa wachimbaji wadogo huku kituo kikijiendesha kwa tija.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa STAMICO, Bw. Deusdedith Magala, alibainisha kwamba, Shirika limekuwa likisimamia kituo hicho kwa karibu ili kuhakikisha walengwa wa kituo hicho wanapata elimu na kunufaika na uwepo wa kituo hicho.

Tayari wachimbaji wadogo sita wanaanzisha mitambo yao ya kuchakata dhahabu katika maeneo yao baada ya kujifunza kutoka kituo cha STAMICO. Aidha Mkurugenzi alibainisha kwamba Shirika lipo katika hatua za kuboresha uwezo wa mitambo ya uchakataji madini kutoka kiwango cha sasa ambacho ni tani 10 kwa siku hadi hadi tani 30 kwa siku hatua ambayo itaongeza ufanisi na kutatua changamoto ya foleni ndefu iliyopo kwa sasa ya kupata huduma katika kituo hicho.