Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

KIJIJI CHA STAMICO CHATWAA TUZO 4 KATIKA MAONESHO YA MADINI MKOANI GEITA


Kijiji cha STAMICO kimepokea jumla ya Tuzo 4 kwa siku ya leo tarehe 27 Septemba, mbili zikiwa zimeenda STAMICO na mbili kwa Vikundi vya TAWOMA na TANZANIA YOUTH IN MINING (TYM).

STAMICO imepokea tuzo mbili kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika miradi yake na uwezeshaji wa makundi maalumu katika kushiriki katika mnyororo wa biashara ya Madini.

Zoezi la utoaji Tuzo limefanyika leo katika Ukumbi wa Nyerere unaopatikana ndani ya Viwanja vya maonesho ya Madini vya Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoani Geita na kutolewa na Mha.Zena Ahmed Said Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akiongea wakati wa kupokea tuzo hizo, Mwakilishi wa STAMICO Afisa Masoko ndugu Mark Stepano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Dkt.Venance Mwasse, alisema tuzo hii ni ishara ya Serikali kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Shirika katika kuendeleza, kuongeza na kuwezesha makundi maalumu ya uchimbaji madini nchini.

Akiongea katika utoaji wa tuzo hizo, Mha.Zena Ahmed Said, Katibu Mkuu Kiongozi, SMZ amewapongeza STAMICO kwa kupokea tuzo ya Kampuni ya Wachimbaji Wakubwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika katika miradi ya uchimbaji Makaa ya Mawe, Kokoto , Uchorongaji, Nikeli na Dhahabu.

STAMICO ni mfano wa kuigwa kwa namna inavyosaidia makundi maalumu ya wanawake, vijana, watu wenye ulemavu wa ngozi na Usikivu hafifu. Alishaur umuhimu wa mambo haya kutangazwa ili Watanzania wajue.

Shirika kwa sasa linatekeleza mkakati wake wa kujiendesha kibiashara na kushiriki kikamilifu katika Uchorongaji na uendelezaji miradi yake ya uchimbaji madini ili kutimiza kauli mbiu yake kivitendo ya MASTASHA .

Sambamba na tuzo hizo 4, kiijiji cha STAMICO kimenyakua jumla ya tuzo 6 tangu kuanza kwa maonesho

Maonesho haya ya Madini Mkoani Geita yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan yanategemewa kufika tamati kesho tarehe 28/07/2025 na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu/ Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko