Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

UZINDUZI WA KIWANDA CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YA RAFIKI BRIQUETTES MKOA WA TABORA ENEO LA KILOLENI TAREHE 21 FEBRUARI, 2026 MGENI RASMI NI WAZIRI WA MADINI MHE. ANTHONY MAVUNDE

20 February, 2026

Shirika la Madini la Taifa linatarajia kuzindua Kiwanda cha kuzalisha Nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes  kilichopo Mkoani Tabora katika eneo la Kiloleni tarehe 21 Februari, 2026 , Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde. Kiwanda hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia katika Mkoa wa Tabora na maeneo yake, pia Nishati hiyo itakuwa mkombozi kwa wakulima wa zao la Tumbaku kwani Nishati hiyo ina uwezo mkubwa wa kukausha Tumbaku kwa gharama ndogo kabisa. Tatizo la ukataji wa miti kwa ajili ya kuni za kukaushia Tumbaku litaisha kabisa katika Mkoa huo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo