UHAMASISHAJI KUHUSU MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Ili kuunga Mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutaka watanzania kuachana na matumizi ya mkaa wa miti. Shirika la Madini la Taifa STAMICO limekuja na njia mbadala ya utunzaji wa mazingira na matumizi ya Nishati safi ya kupikia, majumbani, kwenye mataasisi mbalimbali na sehemu za biashara ya chakula.
Ambapo Shirika linatengeneza na kuuza mkaa rafiki unaotokana na makaa ya mawe, amabao unaitwa Rafiki Briquettes.
Kwa kuzingatia maagizo ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwa watanzania wote waachane na matumizi ya mkaa wa kuni ili kulinda mazingira kwa kutokata miti. STAMICO inawataarifu wananchi wote kuwa, bidhaa hii ya Rafiki Briquettes ni salama kwa matumizi, rafiki kwa mazingira, pia ni rafiki na nafuu kwa gharama.