Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

KATIBU MKUU WIZARA YA MADINI ATEMBELEA STAMICO


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo leo tarehe 09, Machi. 2022 ametembelea Shirikia la Madini la Taifa (STAMICO) na kukutana na Menejimeti pamoja na viongozi wa chama cha Wafanyakazi.

Ziara hiyo imelenga kufahamu utendaji kazi wa Shirika pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika hilo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amemshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa kutenga muda wake kuja kutembelea Shirika ili kujuwa shughuli, miradi mbalimbali, mafanikio na changamoto zinazokabili Shirika kwa ujumla.