Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

KATIBU MKUU WIZARA YA UVUVI NA UCHUMI WA BULUU ZANZIBAR AIPA KONGOLE STAMICO KUUNGA MKONO UCHUMI WA BULUU KUPITIA RAFIKI BRIQUETTES


*DKT MWASSE AWAHASA WAJIOLOJIA KUIISHI VISION 2030 KUPITIA MKUTANO WA TGS*

Katibu Mkuu Wizara ya uvuvi na Uchumi wa buluu Dkt. Aboud S. Jumbe tarehe 11 Novemba 2023 ametembelea banda la STAMICO wakati wa ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania (TGS) uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip,Zanzibar.

Wakati akiwa katika Banda la STAMICO Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Zanzibar alipata maelezo ya shughuli mbalimbali za Shirika kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO CPA (T) Dkt. Venance Mwasse.

Aidha Dkt Mwasse alimwelezea Jinsi ya Shirika ilivyoingia Makubaliano (MoU) na Wizara ya Maji,Nishati na Madini kuifikisha nishati hii kwa Wananchi wa kisiwa cha Zanzibar ambapo siku tahere 13 Novemba 2023 kutakuwa na kikao kazi cha Mashirikiano kati ya STAMICO,Wizara ya Maji,nishati na Madini Zanzibar na taasisi zingine za Serikali na wadau kwa ajili ya kujadili njia bora ya kuifikisha nishati hii kwa Wananchi.

Nae Katibu Mkuu Dkt. Aboud S. Jumbe aliwashukuru STAMICO kwa ubunifu mkubwa wa uzalishaji wa nishati hii mbadala ya Rafiki briquettes inayozalishwa kutokana na mabaki ya Makaa ya Mawe na kuitaka STAMICO kushirikiana pia na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika kuhakikisha nishati hii inawafikia Wavuvi na Wakaushaji dagaa ambao wanatumia gharama ni kubwa kutumia mkaa unaotokana na miti kwa ajili ya kukaushia dagaa hivyo kupelekea kutumia mkaa wa miti kwa wingi ambapo inachochea uharibifu wa mazingira nakutaka kwenye kikao hicho cha tarehe 13 Novemba 2023 Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu kujumuishwa kama mmoja ya wadau wakubwa.

Awali akitoa salamu kwa Washiriki wa Mkutano huo Dkt Mwasse aliwasifu TGS kwa ubunifu wa kupeleka Mkutano mkuu Zanzibar ambapo STAMICO imepata manufaa kwa kupata nafasi ya kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Zanzibar Vilevile aliwasifu kwa Mada zinazozungumzia madini ya kimkakati ambapo kwa sasa dunia inahamia uko katika utafiti wa madini hayo.

Vilevile Dkt Mwasse alizungumzia *Dira 2030 Madini ni Maisha na Utajiri* ambapo dhana hiyo inajikita katika kutafuta taarifa za kijiolojia ambapo taarifa za sehemu iliyopo maji, petrol,mafuta,madini na gesi zitafahamika nakuweza kusaidia nchi kwenye shughuli mbalimbali za uchimbaji. Dkt Mwasse aliwahasa Washiriki na Viongozi wa TGS kuiishi dira hii ambayo awali ilipata baraka kutoka Kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan .Aidha STAMICO nayo itaendelea kuiishi dira hiyo na kuhakikisha inafanikiwa.

Mkutano huu wa jiolojia Tanzania ambao umeambatana na Maonesho umefungwa rasmi leo tarehe 11 Novemba 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).