Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

KIJIJI CHA STAMICO CHAWAVUTIA WENGI MAONESHO YA MADINI GEITA


Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ys 7 ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita limekuwa kivutio kikubwa kutokana na ubunifu na ushiriki wa wadau wengi kwenye eneo moja.

Naibu Waziri Mkuu,Mhe. Doto Biteko ambae alifungua maonesho hayo leo tarehe 5 Oktoba,,alitembelea banda la STAMICO ambalo limepewa jina la "Kijiji cha STAMICO na Wadau"na kuvutiwa na jinsi washiriki walivyojipanga kwa bidhaa mbalimbali kwenye sekta ya madini.

Aliupongeza uongozi wa Shirika kwa juhudi hizo na kutoa rai kuwa liendelee kuwalea wachimbaji wadogo.

Pia alivutiwa na teknolojia mpya ya uchorongaji na uchenjuaji wa madini ambayo ni rahisi kutumia kwa wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa STAMICO. imeendelea kufanya mageuzi makubwa kwenye sekta hiyo na hasa wachimbaji wadogo.

Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA),Bw John Bina ametembelea banda la STAMICO alivutiwa na ushiriki wa vikundi vingi ndani ya banda moja.

Vikundi ambavyo vimealikwa na STAMICO na kushiriki ndani ya banda moja ni pamoja na FEMATA,TAWOMA, TAMAVITA,FDH,Tanzania Youth Miners na Chama cha Wachimbaji Geita (GEREMA).

Wengine ni pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia Geita na Chama cha Wanawake Geita (GEWOMA)

Akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi,Mkurugenzi Mtendaji STAMICO,Dkt. Venance Mwasse amesema kuwa Shirika limefanya mageuzi makubwa katika shughuli zake,hivyo kuweza kujiendesha kwa kulipia gharama mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujilipa mishahara.

Amesema kuwa STAMICO inajivunia kufanya kazi na vikundi mbalimbali vya wachimbaji wadogo na kuongeza kuwa Shirika litaendelea kuvilea hivi vikundi.

Dkt. Mwasse pia ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imedhamiria kuwaleta wachimbaji wadogo pamoja