Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MAGEUZI YA KIUTENDAJI YA STAMICO YAIKOSHA BODI YA BOT


Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) waipongeza STAMICO kufuatia mabadiliko ya kiutendaji yalifanyika ndani ya Shirika hilo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Ngosha Magonya wakati walipotembelea banda la STAMICO katika ziara aliyoifanya kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar Januari 17, 2024.

Amesema, ni jambo la kujivunia kwa Taifa kuona STAMICO inafanya vizuri na inaendelea kukua katika utendaji wake hasa katika kipindi hiki kifupi kufanikiwa kuwa na miradi inayoonekana na kuleta tija kwa Taifa.

Ameitaka STAMICO kuongeza kasi katika kuwasaidia wachimbaji wadogo hususani katika suala la utafiti wa madini ya Dhahabu,hasa kutokana na umuhimu wa madini haya katika kuchangia pato la Taifa.

Akaendelea kwa kusema ni vyema STAMICO ikatumia wataalamu wake wa Jiolojia kuwafikia wachimbaji wadogo katika maeneo yao ili kujua changamoto zao za kijiolojia. Hasa ukizingatia kuna idadi kubwa ya watanzania wanaojishughulisha na uchimbaji mdogo.

STAMICO ipeleke wataalamu wa jiolojia katika maeneo wachimbaji ili kuwasaidia wale wachimbaji wenye maneo mazuri lakini hawana uwezo wa kulipia gharama za utafiti. Kwa kuzingatia eneo kubwa la Tanzania wachimbaji wadogo wanachimba bila kuwa na utaalamu wa miamba.

Aidha ametoa shime kwa STAMICO kuendelea kutoa elimu hata katika maeneo yao ili waweze kujua kuhusu uchimbaji salama unaotunza mazingira ili waweze kuinufaisha nchi.

"Hongereni sana kwa kutumia fursa ya maonesho kutoa elimu, elimu hii pia ikatolewe kwa wachimbaji wadogo huko walipo ili waweze kuona namna Serikali inavyotatua changamoto zao za kiuchimbaji".alisisitiza Magoya

Aidha ameitaka STAMICO kuendelea kujitanua ili kuweza kushughulikia masuala yote ya wachimbaji wadogo katika maeneo husika. Kwa namna wachimbaji wadogo walivyotawanyika nchini ni muda muafaka kwa Shirika kuwa na ofisi ili kuwahudumia wachimbaji kwa ukaribu zahidi.

Akiongea kwa upange wa STAMICO bw. Mark Stephano amesema Shirika limeendelea kujiimarisha katika kuendesha miradi yake, kuwasaidia wachimbaji wadogo na kuhakikisha huduma za uchorongaji zinawafikia.