Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MAKUBALINO BAINA YA STAMICO NA GF TRUCKS YA KUSAIDIA WACHIMBAJI WADOGO YAZAA MATUNDA


Makubaliano yaliyofanyika katika ya STAMICO na kampuni ya GF Trucks Aprili 2023 yameanza kuzaa matunda na kupelekea GF Trucks kuanzishwa kwa ofisi yake ya kuuzia magari na vifaa vya uchimbaji Mkoa wa Geita.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya GF Trucks Mkoa Geita Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde amesema amefurahi kuona Serikali kupitia STAMICO inatekeleza makubaliano yaliyofanyika na kuitaka STAMICO kuzidi kutekeleza kwa vitendo makubaliano yote yaliyofikiwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse ameeleza kuwa chimbuko la ofisi hiyo, ni makubaliano yaliyowekwa Aprili 2023, yaliyolenga kusaidia wachimbaji wadogo kupata vifaa kwa vifaa.

Dkt Mwasse amesema anafurahia kuona GF Trucks wameleta huduma karibu na wachimbaji wadogo jambo litakalorahisisha upatikanaji wa huduma ya Vifaa kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Amesema STAMICO kwa kushirikiana na GF Trucks imebuni njia maridhawa ya kukodisha vifaa ili kutatua changamoto za mtaji wa vifaa kwa wachimbaji

Sambamba na hilo STAMICO imepokea tuzo kutoka GF Trucks kutokana na mchango mkubwa tuliyonya kwa wachimbaji wadogo. Tuzo hiyo alikabidhiwa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse kutoka na ushirikiano uliotukuka wa kati ya STAMICO na Kampuni ya Magari ya GF Trucks.

Dkt Mwasse ameshukuru kwa Kampuni ya GF Trucks kwa kuthamini mchango wa STAMICO katika kuendeleza wachimbaji wadogo na jinsi wanavyo shirikiana katika biashara ya mitambo mbalimbali ikilenga wachimbaji wadogo.

Mwakilishi wa GF trucks ameshukuru ushirikiano uliopo Kati ya STAMICO na GF trucks na ameomba ushirikiano huo uweze kuendelea.

GF trucks wamekuwa wadau muhimu sana wa STAMICO katika mambo mbalimbali kama vile Mkataba wa pamoja wa kuwasaidia wachimbaji wadogo.