Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MD STAMICO ATINGA MAONESHO YA MADINI GEITA, AFURAHIA MWITIKIO MKUBWA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ametembelea katika viwanja vya Maonesho ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita leo tarehe 4 Septemba,2024.

Dkt. Mwasse amepata pia fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya wadau wa sekta ya madini na nishati safi na kujionea teknolojia na bunifu mbalimbali ambazo zimeletwa katika Maonesho hayo ya 7 ambayo hufanyika kila mwaka katika Mkoa wa Geita.

Katika ziara hiyo pia ametembelea banda la Jema Chemicals ambao ni wasambazaji wa kemikali mbalimbali za kuchenjulia dhahabu Mkoani Geita, banda la Geita Gold Mine (GGM) ambapo ameshuhudia teknolojia ya kisasa ya utafutaji,uchimbaji na usafishaji wa madini ya dhahabu.

Alitembelea pia Banda la Wizara ya Madini ambalo limeshirikisha taasisi zilizo chini yake.

Dkt. Mwasse ametumia fursa hiyo kuwapongeza waandaaji wa maonesho haya na washiriki kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imedhamiria kuwaleta wachimbaji wadogo na wakubwa pamoja ili kubadilishana ujuzi na uzoefu katika Sekta hii hapa nchini kuelekea dhima (Vision 2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri.