Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MD WA STAMICO APATA TUZO YA UONGOZI BORA KIPENGELE CHA MASHIRIKA YA UMMA


Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse aibuka mshindi wa Pili na kupata tuzo ya uongozi bora (Recognition Exellency and Leadership). wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa Wakurugezi 100 walofanya vizuri mwaka 2022 wanaotoka kwenye sekta binafsi na sekta ya umma.

Tuzo hizo zimetolewa kwenye Hafla ya kuwatambua na Kuwapongeza Watendaji Wakuu 100 bora nchini Tanzania.(Top 100 Executive List 2022) iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, siku ya tarehe 27 November 2022.

Akiongea wakati wa hafla hiyo mgeni rasmi, Waziri Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar Mhe. Omar Shaaban ametoa pongezi kwa washindi wote na kuagiza kuwa tuzo hizi zikawe chachu kwa watu wanaowaongoza ili kuweza kuleta matokeo chanya katika taasisi zao.

Ametoa wito kwa wote waliopata tuzo hizi, zinatafsiri katika utendaji kazi wao wa kila siku na katika maisha ya Watanzania na kuendelea kuonesha uwezo wao na jitihada za uongozi ili kupeleka bidhaa na huduma hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Amesema ni matarajio yake kuona Watanzania wengi wanakua kitaalamu kupitia Viongozi wao ili kuwafanya waweze kuingia kwenye soko la ajira la kiushindani katika bara la Afrika.

"Kama Waziri mwenye dhamana ningependa kuona tuzo hizi zinatafsiri nafasi ya Tanzania katika soko la kusafirisha (kupeleka) wataalamu nje ya nchi na kuingia katika Ushindani wa ajira Kimataifa." Amesisitiza Mhe. Shaaban

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse amesema anashukuru kupata tuzo hii ya kihistoria kwa Shirika na tuzo hii chachu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Akiongea kwa niaba ya waandaji, Mwanzilishi wa Kampuni ya Eastern Star Consulting Group of Tanzania Ltd. amesema, tuzo hizi zinazotolewa kuhakikisha tunathamini mchango mkubwa unaotolewa na viongozi hawa katika mafanikio ya Taasisi na Kampuni zanazoziongoza.

Amesema tuzo hizi zinalenga kuleta hamasa kwa watendaji kufanya kasi kitaaluma na uongozi madhubuti ili kuleta tija katika maeneo yao ya kazi.

Amesema ili kupata matokeo sahihi yasio na upendeleo wameendesha mchakato huu kwa umakini kwa kusimamiwa na kampuni ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Kimataifa *KPMG*

Aidha Mkurugenzi wa KPMG Bw Alex Njombe amesema walifanya kazi yao kwa uwazi kwa kufuata vigezo vyote walivyopewa na akawapongeza washindi wote na kusema wote wanastahili tunzo hizo.

Tuzo hizo zimetolewa kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City tarehe 27 November 2022 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri Wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe Omary Shaaban.

Zoezi la kutafuta washindi 100 limeratibiwa na Kampuni ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Kimataifa-KPMG.