Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MKAA WA RAFIKI BRIQUETTES WA STAMICO WAMVUTIA WAZIRI KIJAJI


Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Ashatu Kijaji amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa
kuzalisha mkaa mbadala ambao ni suluhisho katika utunzaji wa miti.


Akiwa katika banda la STAMICO wakati wa maonesho ya teknolojia ya Madini Mhe. Kijaji amesema STAMICO imeleta bidhaa mpya ambayo ni mkombozi kwa wananchi na ameishauri STAMICO kuzalisha kwa wingi mkaa huu ili kuhakikisha mkaa unapatikana kila mahali hapa nchini.


Amesema ni wakati sasa wa kuangalia namna nzuri ya kuisambaza teknolojia hii kwa watu wengine ili kuongeza wigo na kasi ya uzalishaji.


"STAMICO mnatakiwa kusambaza teknolojia hii kwa watu wengine zaidi ili waweze kutengeneza mkaa na kuusambaza kwenye maeneo yao na kwa kufanya hivyo STAMICO itaongeza ajira kwa Watanzania" Mhe Kijaji alisisitiza


Akielezea teknolojia ya kutengeneza mkaa huu Meneja wa Masoko na Uhusiano Bw. Geofrey Meena amesema STAMICO imetumia teknolojia ya kisasa ili kufanya mkaa huu uwe rafiki kwa matumizi yake.


Kwa sasa STAMICO imejizatiti kuongeza uzalishaji kwa kuleta mitambo mikumbwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 20, na kwa kuanzia itawekwa katika mikoa ya Pwani na Songwe jambo litakalosaidia kuongeza wigo wa matumizi wa mkaa huu.


Maonesho haya yamefungwa rasmi leo tarehe 8 Septemba 2022.