Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

Mwenyekiti Tume ya Madini aipa Tano STAMICO


Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idriss Kikula leo ameisifu STAMCO kwa kazi nzuri ya ambayo Shirika limefanya kwa kipindi kifupi sana.


Hayo ameyasema leo alipotembelea banda la STAMICO katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba na kujionea jinsi STAMICO inavyojipanga katika na kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakati wa maonesho hayo pamoja na kujionea mirandi na bidhaa mbali mbali za Shirika.


Ameipongeza STAMICO kwa kufikia malengo ndani ya muda mfupi sambamba na kuwaleta pamoja wachimbaji wadogo kutoka mikoa mbalimbali, taasisi za Serikali na kampuni binafsi za madini zikiwemo Twiga Gold, Barick GOLD GEM Tanzanite na vyama vyote vinavyojushughulisha na Biashara ya Madini.


Katika ziara hiyo prof. Kikula alikutana na wachimbaji wadogo wenye usikivu hafifu ambao wamesadiwa mafunzo na vifaa kutoka STAMICO. Aliwashauri kwenda Tume ya Madini ili kutatua changamoto ya utaalamu wa ulipuajikwa miamba.


Ameongeza kuwa na yeye atasaidia kulishughulikia suala hilo kwa kuwaagiza wahusika katika tume ya madini kufika katika mgodi wao, kuwapa mafunzo juu ya ulipuaji ili baadaye waweze kupewe vibali.


Katika ziara hiyo Prof Kikula ameipongeza banda la STAMICO jinsi ya muonekano na mpangilio na jinsi Shirika lilivyowashirikisha wadau wengine kutoka sekta ya umma na binafsi.