Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

NAIBU WAZIRI WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA STAMICO


Leo tarehe 26 Juni , 2024 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ametembelea banda la STAMICO akiwa pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse kwenye maonesho yanayofanyika katika ukumbi wa JKCC, Dodoma wakati wa wiki ya Madini yaliyoandaliwa na FEMATA.

Mhe. Naibu Waziri amewapongeza STAMICO kwa namna inavyosaidia wachimbaji wadogo katika miradi ya uchorongaji kwa kutumia mitambo ya kisasa.

Ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya namna mitambo ya uchorongaji ilivyoleta tija kwa kuwafikia wachimbaji wadogo zaidi ya 30 katika mikoa ya Geita, Mara, Dodoma , Mwanza na Mbeya ambapo zaidi ya Mt 3671.3 zilichorongwa na kuongeza mashapu ya uchimbaji Dhahabu. Taarifa hiyo ilitolewa na Meneja Uwezeshaji Wachimbaj Wadogo, ndugu Tuna Bandoma wakati za ziara ya Mhe. Waziri