Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAFIKI BREQUETTE KUWA SULUHISHO LA MABADIRIKO YA HALI YA HEWA


Mkaa Mbadala wa *Rafiki Brequette* unaozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umekuwa kivutio kwenye Maonesho ya Madini, teknolojia na Vifaa vya Uchimbaji yaliyofanyika katika Jimbo la Jinhua nchini China tarehe 18 Agosti,2023.

Maonesho haya yameenda sambamba na Kongamano la Uwekezaji na Biashara kati ya nchi ya China na Tanzania(*_Tanzania -China Investment and Trade Forum*_) uliowaleta zaidi ya makampuni 100 ya Uwekezaji na Biashara, Utengenezaji na uuzaji wa Mitambo ya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini kutoka Jimbo la Jinhua na majimbo mengine ya China.

Kongamano hilo liliwahusisha pia Viongozi na Watendaji wa Selikali kutoka taasisi mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa shughuli za Uwekezaji, Fedha, Uhamiaji, Forodha na Usafirishaji za China.

Katika Banda la STAMICO, washiriki wa Kongamano hilo walipata wasaa wa kupata maelezo ya shughuli za Shirika na fursa wa Uwekezaji (*Investment Opportunities*) zilizopo kwenye miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika.

Miradi hiyo ni pamoja na Utafiti na Uchimbaji wa Madini ya Kimkakati (*Critical Minerals*), Uchimbaji wa Makaa ya Mawe, Shughuli za Uchorongaji, Uzalishaji wa mkaa mbadala (Rafiki Brequette), nk

STAMICO inashiriki ziara ya Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini zaidi ya 100 wanaoendelea na ziara katika Majibo na Miji mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kuona teknolojia mpya za uchimbaji pamoja na Uwekezaji kwenye vifaa vya Uchimbaji na uongezaji thamani Madini hususani Madini yanayochimbwa Nchini Tanzania.

Aidha, katika maonesho hayo Shirika limeendelea na uhamasisha wa uwekezaji kwenye Madini ya Kimkakati kama *(Lithium , Graphite, Copper)* kupitia leseni za Shirika na za Wachimbaji Wadogo wa Madini.

Kwa upande wa wageni mbalimbali waliotembea banda la STAMICO wamepongeza jitihada za Shirika kwenye kupambana na mabadiriko ya Hali ya hewa kwa kuzalisha Mkaa Mbadala utakaosaidia utunzaji wa mazingira na kuzuia ukataji wa miti hivyo.

Nae *Bw. Khatibu Makenga*, Kansela Mkuu wa Tanzania Jimbo la Guangzhou ameipongeza STAMICO kwa utengenezaji wa Mkaa Mbadala kama nishati ya kupikia kwani hiyo ni jitihada ya kuunga mkoni Serikali na Jumuiya za kimataifa kwenye mapambano dhidi ya Mabadiriko ya Hali ya Hewa Duniani.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa Ziara ya Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini kutoka Tanzania inayoendelea kwenye Majimbo na miji mbalimbali nchini China.