Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAFIKI BRIQUETTES IMEKUWA HABARI YA MJINI MKOANI PWANI.


Leo tarehe 6/10/2022 Katika Maonesho ya 3 ya uwekezaji Mkoani Pwani Mkaa mbadala wa Rafiki briquettes umekuwa kivutio zaidi kwa wakazi wa Mkoa huu.
Wakazi wengi wametoa pongezi kwa uwekezaji mkubwa unaofanywa na STAMICO katika kutatua changamoto ya Nishati ya kupikia na wameomba mkaa uwafikie.
Maneno hayo yamesemwa na wakazi wa Mkoa wa Pwani baada ya kupokea ufafanuzi na faida ya matumizi ya Mkaa mbadala wa Rafiki briquettes kutoka kwa Maafisa wa STAMICO.

Maonesho haya yenye kauli mbiu ya 'Pwani sehemu sahihi ya uwekezaji' yalianza 5/10/2022 na yataisha tarehe 10/10/2022.