Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAFIKI BRIQUETTES YAFIKA KWA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA TAWI LA MTERA NA WAMAMA WAUZA SAMAKI MTERA.


Shirika la Madini linaendelea kutoa elimu ya matumizi ya Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes, Siku ya leo 15 Juni, 2024 STAMICO wakishirikiana na timu ya Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, wamefika kata ya Mtera wilayani Mpwapwa kwa nia ya kutoa elimu ya nishati safi yakupikia ya rafiki Briquettes. Wafanyabiashara wa samaki mtera na Umoja wa Wanawake Tanzania, UWT wamepokea vizuri Mkaa mbadala na baadhi wamenunua na wengine wataendelea kutumia.