Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAIS WA FEMATA AIPONGEZA STAMICO


Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo nchini John Bina ameipongeza STAMICO kwa kuwashirikisha wachimbaji wadogo katika maonesho ya Sabasaba

Amesema ni hatua nzuri iliyofanywa na STAMICO ya kuwapa nafasi baadhi ya wachimbaji wadogo kupitia vyama vyao kuonesha na kuuza bidhaa za madini.

Bina amesema STAMICO imekuwa mlezi mzuri na kuwa sasa inafanya kazi bega kwa bega na wachimbaji wadogo katika kutekeleza adhma ya Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema ushiriki wa huo unatoa fursa kwa wachimbaji wadogo kukutana na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali jambo litakafungua na kukuza soko kwa wachimbaji hao.

Amewataka wachimbaji hao kutumia vizuri fursa hii adhimu ili iweze kuwanufaisha.

Rais wa FEMATA alisema hayo leo tarehe 6 Juni 2022 alivyotembelea banda la STAMICO wakati wa Maonesho ya 46 ya Sabasaba.