Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO KUWAPA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WATU WA MAKUNDI MAALUMU


Shirika la Madini la Taifa STAMICO, limejiwekea malengo ya kuwasaidia watu wa makundi maalumu kama vile walemavu kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa shughuli za kiuchumi kama vile Uwakala wa Usambazaji wa Nishati safi ya makaa ya mawe (Coal Briquet), kuwapa mafunzo ya uchimbaji madini na kuwasimamia ili waweze kunufaika na Rasilimali madini kwa umoja wao.

Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse ameeleza hayo leo Tarehe 8 Aprili 2024 wakati wa Ftari ya pamoja ya Watu wa Makundi maalumu na Watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) iliyoandaliwa na Shirika hilo kwajili watu wa makundi maalumu katika ofisi za STAMICO Jijini Dodoma, ambapo viongozi wa kidini kama vile muwakilishi wa Shekhe wa Wilaya Shekhe Abdurahman ISSA pamoja na Katibu wa Shekhe wa kata, Shekhe Shafii Husein Ramadhan

“Hii sio mara ya kwanza kwa Sisi kufanya hivi kufuturisha watu wa makundi maalumu kipindi hiki cha mwezi Mtukufu tayari tumafanya hivyi Mkoa wa Lindi Kabla ya kufanya leo Jijini Dodoma, na hatuishii tu kuwapa chakula bali tunawapa mafunzo, na fursa za kiuchumi kama vile uwakala wa usambazaji wa Nishati safi, kuwajengea uwezo wa kushiriki kwenye shughuli za Madini kwa kuwapa mafunzo na kuwasimamia nao waweze kunufaika na Rasilimali hizi za Madini”, alisema Dkt Mwasi.

Aidha Dkt. Mwasi ameeleza kuwa tayari STAMICO wamewawezesha Wasikivu hafifu mkoa wa Geita kupata mafunzo ya uchimbaji Madini na kuwapa leseni ya uchimbaji Madini ya Dhahabu kwenye Mgodi uliopo Masumbwe, Geita, na Shirika linaendelea kuwasimimamia ili waweze kunufaika na Rasilimali hiyo ya Madini.

Muwakilishi wa Sheikh wa Wilaya Sheikh Abdurahman Issa amewapongeza Shirika la Madini la Taifa na kuwaomba kuendelea na utaratibu huo kwani wanafanya jambo zuri kwa Jamii hiyo ya watu wenye Makundi Maalumu na ni sambamba na matakwa ya Mwenyezi mungu.