Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO KUWAWEZESHA WATU WENYE UHITAJI MAALUMU


*Dodoma*

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse, ametembelea banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Madini yanayoendelea katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye mahojiano na vyombo vya Habari wakati alipotembelea banda hilo Dkt. Mwasse amesema, STAMICO imedhamiria kuwawezesha watu wenye Ualbino pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.

Aidha Dkt. Mwasse ametoa wito kwa jamii kuachana na dhana potofu za kuwakatisha maisha watu wenye ualbino kwaajili ya Imani za kishirikina ikiwa na wenyewe wanahaki ya kuishi na kupata huduma za kimsingi pamoja na kufanya kazi za kijamii kwa kushirikiana na jamii inayo wazunguka.

Kwa upande wake Maiko Salali ameishukuru STAMICO kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na dhana potofu pamoja na kuwapatia Kontena ili waweze kuuza mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes.