Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO MSHINDI WA KWANZA TAASISI WEZESHI KATIKA SEKTA YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imeibuka kidedea na kuwa mshindi wa kwanza katika Taasisi wezeshi katika Sekta ya Madini.


STAMICO imejinyakulia Ushindi wakati wa kufunga maonesho ya teknolojia ya Madini mkoani Geita baada ya kuonesha bidhaa mpya na mchango wake kwa wadau wa madini nchini.


Akiongelea ushindi huo Meneja wa Masoko Bw. Geofrey Meena amesema STAMICO imekuwa mstari wa mbele katika kuja na bidhaa mpya za ubunifu na kuwasaidia wachimbaji wadogo ili waweze kukuwa kwenye sekta ya Madini.


Kikombe cha ushindi kimekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa maonesho hayo.


Shirika linajivunia ushindi huo umeenda sambamba na sherehe za miaka 50 tangu kuazishwa kwa Shirika.