Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO WASAINI MKATABA MNONO NA MGODI WA BUHEMBA GOLD COMPANY na HATI YA MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA ACME PLC.


Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Dotto Biteko ameshuhudia utiaji saini mkataba ya uchorongaji kati ya STAMICO na Mgodi wa Buhemba Gold Company Ltd na hati ya Makubaliano ya utafiti na uendelezaji madini na kampuni ya ACME PLC.

Kandarasi hiyo ni ya kuchoronga mita 10,000 ya DD na Mita 30,000 za RC. Mkataba huu wa uchorongaji unaotegemea kuingizia Shirika jumla ya TZS bilioni 11.5.

STAMICO vilevile imesaini hati ya makubaliano ya utafiti na uendelezaji wa madini na kampuni ya ACME yenye thamani kati ya dola za kimarekani milioni 300.

Mikataba hiyo miwili imesaniwa tarehe 27 Februari 2022 jijini Dubai, Falme za Kiarabu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.