News
STAMICO YABAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA MADINI ZANZIBAR
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lashiriki maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar ili kuonesha fursa za uwekezaji zilizopo ndani ya Shirika.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse wakati wa ziara yake aliyoifanya katika viwanja vya Maonesho vya Nyamanzi yaliyoanza tarehe 7 hadi 19 Januari 2024.
Akiongea wakati ametembelea banda la STAMICO Mhe. Mohamed Habib Mnyaa Mbunge Mstaafu (CUF) wa Mkanyageni ameipongeza STAMICO kwa kuleta mkaa huo Zanzibar na kuhimiza kuwepo kwa mashirikiano baina ya STAMICO na Wizara ya Nishati Maji na Madini ya Zanzibar ili kuondoa vizuizi katika usafirishaji wa mkaa.
Ameishauri STAMICO kuzalisha kwa wingi ili kuhakikisha muendelezo wa upatikanaji wa mkaa huo.
STAMICO inatumia fursa ya maonesho haya kutangaza Nishati mpya ya Kupikia ya Rafiki Briquattee kwa Wananchi wa Zanzibar ili waweze kuanza kuitumia.
STAMICO imeshiriki maonesho haya ikiwa ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali zitakazofanywa na Shirika baada ya kusaini Mkataba wa ushirikiano kati ya STAMICO na Wizara ya Maji, Madini na Nishati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar