Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAENDELEA KUWAINUA WACHIMBAJI WADOGO NCHINI


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeingia makubaliano na Kampuni ya Meta Plant Equipment ikihusisha uuzaji wa mitambo ya Uchorogaji pamoja na kuwajengea uwezo kuwa Wachimbaji bora.

Makubaliano hayo imefanyika Mbele ya Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde.

Kupitia hafla hiyo MD wa STAMICO Dr. Venance Mwasse ameendelea kuwahakikishia wachimbaji wadogo kuwapa ushirikiano kutoka STAMICO na kuahidi kuendelea kutatua changamoto zinazo wakabili.

MD wa STAMICO aliendelea kueleza manufaa ambayo wachimbaji watayapata kupitia Makubaliano haya ni pamoja na kukodi au kununua mitambo hiyo yenye ubora na kwa bei nafuu zaidi, kupata mafunzo endelevu ya namna ya kutumia mitambo hiyo na kuchoronga.

Mwishoni Dr.Mwasse aliviimiza vyama vya uchimbaji madini nchini kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya wachimbaji kwa kuwa tayari Shirika limeshatoa fedha za kutosha kuhakikisha benki hiyo inaanza kabla ya mwaka wa fedha 2023/24