Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAHAMASISHA WANAWAKE KUSHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewahamashisha wanawake kupitia

Kikundi cha Wanawake na Samia cha Mkoani Geita kushiriki katika suala nzima la utunzaji Mazingira.

Akizungumza kwenye Maonyesho ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita Mkurugenzi Mtendaji wa Dkt. Venance Mwasse amesema STAMICO imekuwa bega kwa bega na kikundi hiki kwa kuwapa kazi ya kutunza miti ili kuhakikisha wanawake wanasimama katika nafasi yao katika kutunza Mazingira

Amesema STAMICO iko tayari kushirikiana na kikundi hiki na inatarajia kutoa uwakala wa kuuza mkaa huo wa Rafiki Briquettes ili kuleta hamasa kwa wanawake wengine kwa kuwa wao ndio watumiaji wa moja kwa moja.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake na Samia. Bi Adelina Kabakana amesema STAMICO wamewezesha zoezi la kupanda miti 560 katika Mkoani Geita ambayo wanaendelea kuitunza kwa maslahi ya nchi.

"Tunajua kwamba mazingira yakiharibika mwanamke ndio anaoathirika kwanza "amesema Kabakama.

Sambamba na haya Bi Kabakana amesema STAMICO imewasaidia katika harakati za kupinga ukatili wa kujinsia kwa kuwatafutia shughuli za kuwapatia kipato na kuwatoa kwenye utegemezi hali iliyokua inapelekea wanawawake hao kuingia kwenye ukatili.

Amesema STAMICO inatarajia kuwapa Wakala wa Nishati Mbadala ya kupikia ijulikanayo kama Rafiki Briquettes, kwa Mkoa wa Geita Jambo litakalowawezesha kujipatia Kipato na kupunguza utegemezi.

Meneja Masoko wa STAMICO Bw. Geofrey Meena akizungumza kwa upande wa STAMICO alisema, STAMICO itakuwa tayari kufanya kazi na kikundi hiki ili kiweze kufikia malengo waliyojiweke kwa kuwapatia bidhaa bora na safi na salama ya kupikia - Rafiki Briquttes.