News
STAMICO YALETA MKAA MBADALA (RAFIKI BRIQUETTES) KWENYE MKUTANO MKUU WA10 WA CCM, DODOMA
Mkaa huo umewavutia wajumbe na kuwafanya waweze kutembelea banda la STAMICO kwa wingi ili kufahamu zaidi kuhusu mkaa ambao umekuwa rafiki na salama kwa matumizi ya majumbani.
Akitoa elimu kwa wadau kuhusu mkaa huo, Mhandisi Mbaraka Haruni amesema Mkaa huo ni mzuri kwa kuwa umetengenezwa kwa umakini mkubwa ili kuepusha athari za kiafya na kimazingira.
Haruni ameongeza kwamba Shirika limeweka bei nafuu ili kila mtanzania aweze kununua Mkaa huu.
Baadhi ya wadau kutoka Zanzibar walisema wamevutiwa sana na mkaa huo kwani ni mzuri na wakaonesha nia ya kuwa mawakala wa mkaa huu wa STAMICO kwa upande wa Tanzania Visiwani.
"Nimevutiwa sana na mkaa huu naomba STAMICO iangalie namna ya kuupelekea Zanzibar kupitia wao au mawakala" Alisisitiza Bi Suliha Mzee, Katibu Umoja wa Wanawake Tanzania upande wa Zanzibar.
Mkutano huu umefanyika katika mkoa wa Dodoma kwa siku mbili mfululizo, Disemba kuanzia tarehe 7 na kukamilika 8, 2022.