Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAZIDI KUDADI FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWENYE UCHIMBAJI WA MADINI YA KIMKAKATI NA MAKAA YA MAWE TANZANIA


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeendelea kunatangaza fursa za Biashara na Uwekezaji kwenye Madini ya Kimkakati na Makaa ya Mawe kupitia leseni zake na leseni za Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini Tanzania.

Fursa Hizi zimetangazwa katika Makongamano ya Uwekezaji na Biashara yaliyofanyika tarehe 20 na 21 Agost, 2023 katika miji ya Jining na Tai ‘an katika Jimbo la Shadong ambalo ni maarufu kwa viwanda vya utengenezaji wa Vifaa vya Uchimbaji wa Madini.

Katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika katika Hotel ya Ramada Plaza Mji wa Tai an ambapo Uongozi wa Mji wa Tai An na Wafanyabiashara na wetengenezaji wa Mitambo na Vifaa mbalimbali vya Uchimbaji wamehudhuria.

Katika Kongamano hilo Bw. Denis Silas Mjiofizikia STAMICO amefanya mazungumzo na Makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni la Shandong Energy Equipments Group watengenezaji wa Vifaa vya Uchimbaji wa Makaa ya Mawe.

Kampuni hilo linalomilikiwa na Serikali ya Jimbo la Shandong liko tayari kuingia kwenye Makubaliano na STAMICO kwenye upande wa Vifaa vya Uchimbaji wa Makaa ya Mawe.

Naye Bi. Shao Yuanyuan Mhandisi Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kimataifa wa Kampuni Shandong Energy Equipments Group alisema wako tayari kushirikiana na STAMICO hasa kwenye upande wa Vifaa vinavyotumika katika Uchimbaji wa Makaa ya Mawe.

STAMICO imeendelea kutumia ziara hiyo kutafuta fursa zitakazokuwa na manufaa kwa Wachimbaji wadogo ili kuleta mabadiliko katika sekta ndogo ya uchimbaji mdogo.