Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YANG’ARA YABEBA TUZO MBILI


SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeng'ara katika kikao kazi cha Wenyeviti na Watendaji wa Mashirika ya Umma baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Taasisi za umma zilizofanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji na yenye tija kwa mwaka 2023. (Turn Around Company in Financial and Operational Performance as of June 2023)

Pia STAMICO imenyakua tuzo ya pili katika kundi la mashirika ya umma ambayo yametoa gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. (Outstanding Dividends payment SOE Category as of June 2023.

Tuzo hizo zimekabidhiwa leo jijini Arusha na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyefungua kikao kazi hicho na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Venance Mwasse pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya STAMICO, Meja Jenerali (Mstaafu) Michael Isamuhyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameipongeza STAMICO na kubainisha kuwa katika miaka miwili iliyopita ilikuwa inafikiriwa kufutwa kutokana na utegemezi lakini sasa wameweza kuchangia hadi gawio kwenye mfuko mkuu wa Serikali.