Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YANGARA AFRICA, YANYAKUWA TUZO YA ACOYA


Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) limenyakuwa tuzo kama Kampuni bora ya mwaka Africa kwenye sekta ya Madini 2023 (Mining Company of the Year Award 2023). Tuzo hiyo imetolewa katika hafla yaliyofanyika Mlimani City Dar es Salaam tarehe 4 Agosti 2023

Mwaka huu 2023 ndio mara ya kwanza tuzo hizo kutolewa Tanzania na zinajulikana kama ACOYA (Africa Company of the Year Awards).

Zaidi ya nchi 15 kutoka bara la Afrika zilishiriki kwenye mashindano haya na STAMICO kuibuka kidedea kama Kampuni Bora ya Madini Africa.