Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAPELEKA NISHATI MBADALA WILAYA YA MBINGA KUNUSURU MISITU


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kutanua wigo kwa watumiaji wa mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes kwa kuamua kushirikiana na Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga kwa kupeleka mkaa katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Aziza Ally Mangosongo Aman Makolo Mbinga Vijijini.

Imeelezwa kuwa ni jitihada za makusudi za STAMICO kuhakikisha linazalisha mkaa mbadala kwa wingi na kuhamasisha matumizi yake katika maeneo mbalimbali za nchi ili wananchi wapate uelewa wa Nishati hii ya kupikia na kuachana na nishati zinazotokana miti ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakioneshwa kufurahishwa na jitihada hizo za kutunza mazingira Waheshimiwa Madiwani waliotembelea banda la maonesho wameipongeza STAMICO kwa kubuni mkaa huku wakiishuru Jumuiya ya Wazazi kuupokea mkaa huo mbadala kama moja ya miradi yao.

Akiongea kwa niaba ya Madiwani wa Mbinga DC Mheshimiwa Diwani Ambrose Nchimbi amesema ni jambo la kheri kuona taasisi ya Serikali inashirikiana na Jumuiya ya wazazi kuunga mkono jitihada za kupambana na suala la uharibifu wa mazingira,

" Tunatoa pongezi kwa STAMICO na Jumuiya ya Wazazi kwa kubuni na kuuchukua mradi huu wa mkaa mbadala ili kuhamasisha jitihada za makusudi za kuhifadhi misitu". Alisema Mhe. Nchimbi.

Aidha ameimeomba STAMICO kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati mbadala ya kupikia ili kwa wakazi wa Wilaya ya mbinga waweze kupunguza matumizi ya mkaa utokanao na miti.

Akiongea kwa upande wa STAMICO Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bibiana Ndumbaro amesema mkaa huu umetengenezwa kwa kuzingatia usalama wa mtumiaji sambamba na mazingira na unapatikana kwa bei nafuu.

Ameushukuru uongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Mbinga kwa kuamua kuweka mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes kama moja ya miradi yao na kuongeza kuwa STAMICO itaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha watu wanahamasika kutumia mkaa mbadala ili kutunza mazingira.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bi. Hajiri Kapinga amesema Jumuiya hiyo wamejipanga vyema kuusambaza mkaa na kuhakikisha wana Mbinga wanaanza kutumia mkaa huu.

"Tumeitika wito wa Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan wa kutumia mkaa mbadala ili kuweza kutunza mazingira. Hivyo tumeifanya kuwa moja ya miradi ya maendeleo ndani ya Jumuiya ya wazazi wilaya ya Mbinga.

Mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes ni nishati mbadala ya kupikia inayotengezwa kwa lengo la kupunguza ukataji miti ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.