Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YASAINI MKATABA MNONO WA UCHOROGAJI WA ZAIDI YA BILLIONI 55 NA MGODI WA GGML.


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika shughuli za uchorongaji madini kwa kuweza kusaini mkataba mnono wa kuchoronga na mgodi mkubwa na Geita Gold Mine (GGML) uliopo Geita.

Mkataba huo unathamani ya Billioni 55.2 na umetiwa saini Machi 27 2023 Mkoa wa Geita mbele ya Viongozi wa Wizara ya Madini na Mgeni rasmi Waziri wa Madini Mhe. Dkt.Doto Biteko

Mhe Waziri ameipogeza STAMICO kwa hatua ya kupata kandarasi kubwa na akasisitiza kufanya kazi hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa kwa kipindi chote cha mkataba ili kuwavutia makampuni wengine.

Amewapongeza pia Kampuni ya GGML kwa kuwa mstari wa mbele katika kuzingati sheria ya local content kwa kuwa wanashirikisha wazawa katika kupata kandarasi katika mgodi wa GGML.

“Nimefurahi kuona Kampuni za wazawa wakipata kandarasi kama hizi hapa nchini tofauti na hapo kipindi cha nyuma waliokuwa wanapata kandarasi ni makampuni ya kigeni” alisema Mhe Waziri

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema mkataba huu ni udhibitisho kuwa watanzania wanaweza kushiriki kikamilifu katika kandarasi zinatokea katika mnyororo wa thamani wa madini.

Ametaja mafanikio makubwa ya mkataba huo ni pamoja na ongezeko la mapato kwa Shirika na kuongeza ajira kwa Watanzania “Tunajivunia kufanya kazi na GGM kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu kwa mfululizo na kwa kipindi chote tumekuwa na ushirikiano mzuri. Mgodi wa GGM umekuwa mfano wa kuigwa katika kuthamini na kuamini Kampuni za Kitanzania kufanya kazi za uchorogaji (local content) hivyo kumesababisha kupata tena kandarasi nyingine kubwa kama hii”

Kwa upande wa Mgodi wa GGML Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw.Damon Elder amesema wanajivunia kufanya kazi na STAMICO na wamekuwa wakifanya za kazi uchorongaji kwa kiwango cha juu sana na hivyo kuwa shawishi na kuwapa kandarasi nyingine kubwa kama hii.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo ameishukuru Wizara ya Madini, Viongozi na wananachi wa Mkoa wa Geita kwa ushirikiano wanaoutoa kwa STAMICO.

Amesema STAMICO haitasita kuwachukulia hatua wale wote ambao wataonesha dalili za makusudi za kurudisha nyuma jitihada au kukwamisha matokeo chanya kwa Shirika.

Tukio hilo la utiaji saini ulilitanguliwa na tukio la upandaji Miti na utoaji vifaa kwa wachimbaji wadogo wenye uhitaji.