Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YASHIRIKI JUKWAA LA PILI LA USHIRIKISHWAJI WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki katika Jukwaa la Pili la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content Forum) lililoandaliwa na Tume ya Madini jijini Arusha kuanzia tarehe 15 hadi 17 Machi, 2023.

Jukwaa hili lilikua na lengo la kuwakutanisha kwa pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya madini ili kujadili namna bora ya kuongeza ushirikishwaji wa watanzania katika shughuli za madini.

Kauli mbiu iliyoongoza jukwaa hili ni ‘’ Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini kwa kufunganisha na Sekta nyingine kwa uchumi imara wa Tanzania’.

Mgeni rasmi katika jukwaa hilo alikua Mhe. Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa na ambaye alizindua rasmi mfumo wa kuandaa na kuwasilisha taarifa za Local content na CSR kwa njia ya kielektroniki uitwao LCCSR system.

Kwa upande mwingine wadau mbalimbali walitoa pongezi kwa STAMICO kwa kuwa Mdau muhimu anayefanya vizuri katika Sekta ya madini kwa ushirikishaji wake Jamii katika sekta hiyo.

Aidha, Mkrugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geofields (TZ) Ltd Bw. Dennis Dillip alilieleza jukwaa ni kwa namna gani wao kama Kampuni ndogo inayotoa huduma za uchorongaji inavyohamasishwa na STAMICO kwa jinsi inavyofanya shughuli za uchorongaji kiufanisi na kwa kuzingatia usalama ‘safety compliance’ hususani katika Mgodi wa GGM. Aliendelea kulieleza jukwaa kwamba wanaiona STAMICO kama moja ya Makampuni Makubwa ya Uchorongaji Tanzania yenye uwezo wa kushindana na makampuni makubwa ya uchorongaji duniani.

Pia, Wadau wengine kama NMB walieleza jinsi gani wanavyoshirikiana na STAMICO kwenye kuwasaidia wachimbaji wadogo waweze kufikia lengo la kukopesheka na kuongeza mitaji yao ili kuendelea kusupport dhana nzima ya ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini.

Jukwaa hilo lilifungwa rasmi tarehe 17 Machi, 2023 na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Proffessa. Idris Kikula ambapo STAMICO ilipata cheti cha utambuzi kama mmoja ya wadhamini wa jukwaa hilo.