News
STAMICO YASHIRIKI JUKWAA LA TATU LA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) leo tarehe 22 Mei 2024 limeshiriki jukwaa la tatu la ushirikishwaji Watanzania katika Sekta ya Madini linalofanyika Jiji Arusha kuanzia tarehe 22- 24 Mei 2024.
Mgeni rasmi wa jukwaa hilo Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde ameipongeza STAMICO kwa kushiriki vizuri katika kuinua sekta ya Madini na kuchangia pato la Taifa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ameelezea jinsi Shirika lilivyopata mafanikio makubwa katika dhana ya ushirikishwaji Watanzania kupitia Miradi yake, bidhaa na huduma inazotoa.
Aidha kupitia jukwaa hilo wageni mbalimbali waliweza kutembelea banda la STAMICO kujionea bidhaa na shughuli za Shirika.
Aidha jukwaa hilo linaenda sambamba na Maonesho ya Madini ambapo taasisi mbalimbali toka sekta ya umma na sekta binafsi zinashiriki. Mkutano wa jukwaa hilo unatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 24 Mei 2024.