News
STAMICO YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA AFRIKA YA KUSINI
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeendelea na juhudi za kutangaza fursa za uwekezaji kwa kushiriki katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika ya Kusini, lililofanyika tarehe 15 hadi 16 Machi, 2023 huko nchini Afrika Kusini.
Ushiriki wa STAMICO katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji umeenda sambamba na ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassa ambaye aliambatana na Viongozi wa wizara Mbali mbali akiwemo waziri wa Madini Dkt Doto Biteko
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse, katika Majadiliano ya kisekta ameeleza fursa iliyopo ya uwekezaji katika sekta ya madini huku akiyakaribisha nakampuni ya madini na utengenezaji wa mitambo ya uchenguaji dhahabu yaliyopo Afrika Kusini kuja kuwekeza Tanzania.
Katika Kongamano hili Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhe Mr Kheri A. Mahimbili na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili Dkt. Hassan Abbas ni miongoni mwa Viongozi wa Serikali walitembelea Banda la STAMICO pia ikumbukwe Kongamano hili limehudhuriwa na makampuni zaidi ya 350 kutoka Africa ya Kusini yakiongozwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.